IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mfalme wa Malaysia awaenzi washiriki wa Mashindano ya Kimataifa wa Qur'ani

12:27 - October 10, 2024
Habari ID: 3479568
IQNA - Mfalme na Malkia wa Malaysia wameandaa hafla ya chai ili kuwaenzi washiriki na majaji wa Mkutano wa 64 wa Kimataifa wa Kuhifadhi na Kusoma Qur'ani ya Malaysia (MTHQA).

Sultan Ibrahim na mkewe Malkia Raja Zarith Sofiah walihudhuria hafla hiyo siku ya Jumatano.

Ilifanyika katika Ukumbi Mkuu wa Karamu ya Istana Negara huko Kuala Lumpur na kuhudhuriwa na wahifadhi na wasomaji 92 wa Qur'ani kutoka nchi 71 wanaoshindana katika MTHQA.

Pia walikuwepo wajumbe wa jopo la majaji, Waziri wa Masuala ya Kidini wa Malaysia Mohd Na’im Mokhtar na baadhi ya maafisa wengine wakuu.

Mashindano hayo ambayo hujulikana rasmi kama Mkusanyiko wa Kimataifa w Kuhifadhi na Kusoma Qur'ani Malaysia (MTHQA) yalianza katika hafla iliyosimamiwa na Waziri Mkuu Anwar Ibrahim mnamo Oktoba 5.

Washindani hao wanashindana katika kategoria mbili za usomaji na kuhifadhi Qur'ani.

Sherehe ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa kategoria hizo mbili imeratibiwa kusimamiwa na mfalme na malkia wa Malaysia Jumamosi, Oktoba 12.

.

Malaysia King Honors Participants in Int’l Quran Contest  

Malaysia King Honors Participants in Int’l Quran Contest  

3490213

captcha