IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Ufafanuzi wa vigezo vya majaji katika Shindano la Int'l Quran la Malaysia

21:22 - October 12, 2024
Habari ID: 3479581
IQNA – Vigezo vinavyotumiwa na majaji katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia vimeimarika mwaka huu, afisa mmoja alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kiislamu Malaysia (JAKIM) Sirajuddin Suhaimee maamuzi ya majaji katika  Mashinano ya 64 ya Kimataifa ya Kuhifadhi na Kuhifadhi Qur'ani (MTQHA) yamefanyika kwa uwazi.

Sirajuddin, ambaye ni mwenyekiti wa jopo la majaji katka mashindano hayo, amesema kuwa ingawa miongozo ya majaji ilibaki sawa na miaka iliyopita, baadhi ya vipengele vya vigezo vinavyotumika vimeimarishwa.
"Mchakato wa tathmini unajumuisha vipengele vya Tajweed, Fasahah (ufasaha), ubora wa sauti, na usahihi wa hifdhi. Hii ni kazi yenye changamoto inayohitaji utaalamu maalum," amesema.
Alipoulizwa kuhusu mchakato wa tathmini ya majaji kutoka katika chumba cha majaji, alisema majaji hao hawajui utambulisho wa washiriki, ikiwa ni pamoja na nchi yao ya asili au sura.
"Majaji hutathmini tu kulingana na kile wanachosikia bila kujua washiriki ni nani ili kuhakikisha uwazi katika hukumu na kuepuka upendeleo wowote."
Mashindano ya mwaka huu ina majaji 15 kutoka nchi mbalimbali, ikiwabakiza majaji kutoka mataifa kama Morocco na Uturuki huku ikitambulisha majaji wapya kutoka Saudi Arabia, Indonesia na nchi nyingine jirani.
Mashindano hayo ambayo hujulikana rasmi kama Mkusanyiko wa Kimataifa w Kuhifadhi na Kusoma Qur'ani Malaysia (MTHQA) yalianza katika hafla iliyosimamiwa na Waziri Mkuu Anwar Ibrahim mnamo Oktoba 5 na yanamalizika Oktoba 12.

3490230

Habari zinazohusiana
captcha