IQNA

Jaji wa Iran asisitiza uadilifu katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Malaysia

21:31 - July 23, 2025
Habari ID: 3480991
IQNA – Mtaalamu mkongwe wa Qur’ani, Gholam Reza Shahmiveh, amezungumzia umuhimu wa uadilifu na kuwepo kwa Iran katika jopo la majaji wa Mashindano ya Kimataifa ya Usomaji na Uhifadhi wa Qur’ani ya Malaysia.

 

Kwa mara ya kwanza baada ya karibu miaka 20, Iran itawakilishwa katika jopo la majaji wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Malaysia (MTHQA), ambapo Ustadh Gholam Reza Shahmiveh — mwalimu mashuhuri wa Qur’ani — amealikwa kuhudumu kama jaji katika toleo la 65 la mashindano hayo, yatakayofanyika Kuala Lumpur kuanzia Agosti 2 hadi 9.

“Licha ya nafasi ya kipekee ya Iran katika nyanja ya Qur’ani ndani ya ulimwengu wa Kiislamu, kwa miaka mingi hatujakuwa na mwakilishi wetu katika tukio hili muhimu la kimataifa,” Shahmiveh aliambia IQNA. “Sasa, kilicho muhimu ni kuhakikisha nafasi hii inadumu katika miaka ijayo, InshaAllah.”

Akizungumzia mtazamo wake katika kazi ya kujaji, alisisitiza juu ya uadilifu:
“Daima huwa napima washiriki kwa kuzingatia tu kiwango chao cha usomaji ndani ya mashindano hayo, pasina kuathiriwa na umaarufu au mahusiano ya awali. Kwa mtindo huu, anayestahili zaidi , bila kujali uraia wake, hupata heshima anayostahili,” alisema.

Shahmiveh pia alieleza kuwa mashindano ya Malaysia hayatoi majina ya washiriki wakati wa usomaji, jambo linalosaidia kulinda hali ya kutokuwa na upendeleo.

Aidha, aligusia tofauti za kiufundi katika kanuni za mashindano.
“Katika mashindano ya Malaysia, qari anapaswa kutumia maqamat manne ndani ya muda uliowekwa, hivyo ni lazima wasimamie muda na mpangilio kwa umakini mkubwa.”

Toleo la mwaka 2025 linatarajia kuwa na washiriki 72 kutoka mataifa 50. Iran pia itawakilishwa na qari mashuhuri, Mohsen Qassemi, katika kitengo cha usomaji.

3493954

Habari zinazohusiana
captcha