Qari wa kiume wa Malaysia Muhammad Husaini Mahmur na qari wa kike Nur Hidayah Abdul Rahman walitawazwa mabingwa katika mashindano hayo ambayo hujulikana rasmi kama Mkusanyiko wa Kimataifa wa Kuhifadhi na Kusoma Qur'ani Malaysia (MTHQA).
Muhammad Husaini Mahmur alipata nafasi ya kwanza katika kategoria ya qiraa au kisomo kwa kupata alama 95.71. Abdur Rasheed kutoka Pakistan na Wahyu Andi Saputra kutoka Indonesia walichukua nafasi za pili na tatu, mtawalia.
Kwa upande wa wanawake, Nur Hidayah Abdul Rahman aliibuka bingwa kwa kupata alama 91.76, akifuatiwa na Raihana Ambangaladi kutoka Ufilipino na Syamimi Assahira kutoka Indonesia.
Katika kitengo cha kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa wanaume, Oubaydullah Boubacar Ango kutoka Niger alishika nafasi ya kwanza kwa alama 97.63. Ibrahim Sow kutoka Ivory Coast na Aeimiddin Farkhudinov kutoka Russia waliweza kupata nafasi za pili na tatu.
Katika kitengo cha kuhifadhi kwa wanawake, Habsatou Hamissou Boubacar kutoka Niger alishika nafasi ya kwanza kwa kupata alama 96.13, huku Putri Aminah Mohd Hanif kutoka Malaysia na Fathimah Shaya Zahir kutoka Maldives wakishika nafasi za pili na tatu.
Washindi katika kategoria za qiraa na kuhifadhi walipokea zawadi za pesa taslimu RM40,000 kutoka kwa serikali, vito vya dhahabu vyenye thamani ya RM12,000 kutoka kwa Wakfu wa Kiislamu wa Maendeleo ya Kiuchumi Malaysia (YaPEIM), pamoja na zawadi zingine kadhaa na vyeti.
Mashindano yam waka huu yaliyandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Kiislamu Malaysia (JAKIM), jijini Kuala Lumpur yalikuwa na washiriki 92 kutoka nchi 71.
Majaji wa mashindano hayo walizingatia tajweed, ufasaha, ubora wa sauti, na usahihi wa kuhifadhi.
3490246