IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya 64 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia yameanza leo

17:19 - October 05, 2024
Habari ID: 3479540
IQNA – Toleo la 64 la Mashindano ya Kimataifa la Kuhifadhi na Kusoma Qur’ani ya Malaysia (MTHQA) yamefunguliwa rasmi leo usiku huko Kuala Lumpur.

Mashindano hayo yatashirikisha makundi mawili: kuhifadhi na usomaji wa Qur'ani, kwa mujibu wa Idara ya Maendeleo ya Kiislamu ya nchi hiyo (JAKIM).

Sherehe ya ufunguzi imefanyika  saa tatu usiku kwa saa za huko Kuala Lumpur na imehudhuriwa Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim katika Kituo cha Biashara cha Ulimwenguni cha Kuala Lumpur.

Mashindano hayo yataendelea hadi 12, na vikao vikifanyika asubuhi na jioni. Kategoria ya kuhifadhi itafanyika asubuhi, wakati kitengo cha qiraa kitafanyika jioni.

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia huandaliwa kila mwaka katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Kuala Lumpur.

Jumla ya wawakilishi 76 kutoka nchi 52 walishindana katika kategoria mbili za usomaji na kuhifadhi Qur'ani katika toleo la 63 mwezi Agosti 2023.

 4240664

Habari zinazohusiana
captcha