Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Kidini, Datuk Dkt. Mohd Na’im Mokhtar, amesema kuwa mpango huu hautokomei tu kwenye usomaji wa Qur’an bali unalenga pia kuelewa na kuishi kwa mujibu wa mafundisho yake.
Amesema: “InshaAllah, juhudi hizi zitaimarishwa zaidi, si tu kwa ajili ya kusoma, bali Qur’an ieleweke kupitia kutafakari kwa kina (tadabbur) na itekelezwe katika maisha yetu ya kila siku.”
Akaongeza: “Ujumbe huu si kwa Wamalaysia tu, bali tunakusudia kuufikisha pia katika ngazi ya kimataifa, ulimwenguni kote.”
Waziri aliyasema hayo katika hafla ya Quran Hour iliyoandaliwa kama sehemu ya Mkutano wa Kimataifa wa Usomaji na Kuhifadhi Qur’ani (MTHQA) unaoendelea jijini Kuala Lumpur.
Surah al-Saff ilichaguliwa kama sura kuu kwa hafla hiyo – sura inayohimiza umoja wa Waislamu na kuwataka wasimame pamoja kwa nguvu na mshikamano katika njia ya haki.
MTHQA ni mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya juu kabisa nchini Malaysia, ambayo kila mwaka huwaleta pamoja wasomaji (maqāri’) na wahifadhi (huffādh) kutoka kona mbalimbali za dunia, kwa madhumuni ya kuonyesha ujumbe wa Qur’ani kwa watu wote na nafasi yake ya kiroho katika maisha ya mwanadamu.
Hafla hiyo ilifunguliwa tarehe 2 Agosti na itaendelea kwa muda wa juma moja.
3494128