IQNA

Jinai za Israel

Jeshi katili la Israel lawachoma moto Wapalestina 40 katika shambulio la kinyama Rafah

11:15 - May 27, 2024
Habari ID: 3478890
IQNA-Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel limeshambulia kwa makombora kambi ya watu waliolazimika kuhama makazi yao na kuhamia eneo lililotengwa kuwa na usalama huko Rafah, na kuwaua shahidi Wapalestina wasiopungua 40, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.

Shambulio hilo la linyama la jeshi la Kizayuni katika eneo la Tal as-Sultan limefanywa wakati askari wa jeshi hilo wakishambulia pia kwa makombora makazi ya Wapalestina waliokimbia makazi yao katika maeneo ya Jabalia, Nuseirat na mji wa Gaza na kuua watu wengine 160 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Hayo yanajiri huku Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International likiitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ichunguze jinai na uhalifu wa kivita uliofanywa katika mashambulizi matatu ya hivi karibuni ya Israel yaliyoua raia 44 wa Palestina, wakiwemo watoto 32.

Shambulio hilo la linyama la jeshi la Kizayuni katika eneo la Tal as-Sultan limefanywa wakati askari wa jeshi hilo wakishambulia pia kwa makombora makazi ya Wapalestina waliokimbia makazi yao katika maeneo ya Jabalia, Nuseirat na mji wa Ghaza na kuua watu wengine 160 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Hayo yanajiri huku Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International likiitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ichunguze jinai na uhalifu wa kivita uliofanywa katika mashambulizi matatu ya hivi karibuni ya Israel yaliyoua raia 44 wa Palestina, wakiwemo watoto 32.

3488513

Habari zinazohusiana
Kishikizo: jinai za israel
captcha