Hamas imesema hayo mapema leo Jumanne na kuongeza kuwa, mateka wote wa Kizayuni walioko mikononi mwa wanamapambano wa Kiislamu inabidi waachiliwe huru haraka na warejee kwenye familia zao, lakini Benjamin Netanyahu na serikali yake yenye misimamo mikali ya Kizayuni wanahatarisha usalama wa mateka hao.
Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar imenukuu taarifa ya Hamas ikisema kuwa, Netanyahu ameonesha kuwa hana nia kabisa ya kufikiwa makubaliano ya kusimamisha vita na mabadilishano ya mateka kutokana na matamshi yake aliyotoa alfajiri ya leo Jumanne.
Kwa mara nyingine Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina , Hamas. imesema kuwa, matamshi ya Netanyahu ni ya kuwadanganya wafuasi wake na serikali ya Marekani, madai hayo yamejaa uongo kwani ukitoa mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina, Netanyahu ameshindwa kufanikisha lengo jingine lolote lile.
Harakati hiyo ya muqawama wa Palestina pia imesema, matamshi ya Netanyahu yanaonesha ni mtu aliyekata tamaa, aliyeshindwa na anayetafuta ushindi kwa namna yoyote ile, lakini kamwe hatoupata.
/3489751