IQNA

Pendekezo la uanzishwaji wa Sekretarieti ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran jijini Mashhad 

21:22 - February 16, 2025
Habari ID: 3480227
IQNA – Mtaalam wa Qur'ani wa Iran ametoa wito wa kuanzishwa kwa sekretarieti ya kudumu ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran katika mji mtakatifu wa Mashhad. 

Abbas Salimi, ambaye alikuwa mwendeshaji vikali katika toleo la 41 Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran Mashhad mwezi uliopita, alisema katika mahojiano na IQNA kwamba sekretarieti ya kudumu inapaswa kuanzishwa katika Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS), idara ambayo ni maarufu kama Astane Quds Razavi

"Sekretarieti hii inapaswa kuwa chini ya kuba ya dhahabu ya Haram ya Imam Ridha (AS). Kwa nini? Ili kuwaambia wageni kwamba tunajivunia uwepo wa Imam ambaye, kulingana na hadithi za kweli, alihitimisha Qur'ani kila siku tatu," alisema. 

"Licha ya kubeba majukumu makubwa, Imam huyu mkuu alisoma Juzuu 10 za Qur'ani Tukufu kila siku. Hii inatuma ujumbe kwa Waislamu wote na hasa kwa wale ambao ni viongozi na wanafikiria kwamba wana shughuli nyingi mno kuungana na kushughulika na Qur'ani. Kwa hivyo, Mashhad ina uwezo wa kuendelea kuwa mwenyeji kwa ushirikiano wa Shirika la Wakfu la Iran  na Astane Quds Razavi." 

Alipoulizwa kuhusu wito wa kuanzishwa kwa shirikisho la mashindano ya kimataifa ya Qur'ani duniani kote, mwanaharakati mkongwe wa Qur'ani alisema suala hili kwa sasa liko katika hatua ya kutafakari. 

Salimi aliongeza, "Imam Ali (AS) anasema kwamba kupitia kubadilishana mawazo, njia bora ya uadilifu inaundwa. Ikiwa tunaweza kuinua mashindano haya zaidi ya hali yao ya sasa na kuanzisha shirikisho hili, sekretarieti, au jina lolote litakalokuwa, na kuwa nayo kila miaka michache katika moja ya nchi zinazoandaa mashindano ya kimataifa.”

3491877

Habari zinazohusiana
captcha