IQNA

Bi kizee wa Malaysia wa miaka 117 asherehekea Idul Fitr, aendelea kusoma Qur'ani

20:18 - April 02, 2025
Habari ID: 3480486
IQNA – Bi kizee mwenye umri wa miaka 117, anayeaminika kuwa miongoni mwa wazee zaidi nchini Malaysia, ameonyesha shukrani kwa kuwa na uwezo wa kusherehekea Idul Fitr nyingine akiwa na familia yake.

Kelthum Yaakub, kutoka Pasir Mas, Kelantan, alisherehekea tukio hilo akiwa amezungukwa na familia yake kubwa, inayojumuisha watoto 11, wajukuu 50, vitukuu 30, na vilembwe vine.

Licha ya umri wake mkubwa, Kelthum—anayeitwa kwa upendo Makwa—bado ni mwenye bidii na anaendelea kusoma Qur'ani Tukufu na kufunga katika mwezi wa Ramadhani. 

"Naweza pia kutembea hadi duka lililo karibu," aliambia Bulletin TV3. 

Pamoja na kuendelea na maombi yake, alishiriki mbinu zake za kujisadia kuwa na afya bora, zinazojumuisha kunywa maji ya kutosha na kula ulam, saladi ya jadi ya Wamalay inayotengenezwa kwa mboga mbichi na mimea.

3492549

Habari zinazohusiana
captcha