IQNA

Harakati za Qur'ani

Waziri Mkuu wa Malaysia awapongeza wasanii wa Iran katika uga wa Qur'ani

18:33 - January 29, 2023
Habari ID: 3476483
TEHRAN (IQNA) - Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim alitembelea Tamasha la Kimataifa la Sanaa la Qur'ani Tukufu la Restu, linaloendelea katika nchi hiyo ya Kusini Mashariki mwa Asia.

Akitembelea sehemu tofauti za maonyesho ya tamasha hilo huko Putrajaya, alizungumza na wasanii wa Irani waliohudhuria hafla hiyo ya kitamaduni na kusifu kazi zao za sanaa, ambazo ni pamoja na kazi za uandishi wa kaligrafia ya Kiarabu  na calligraphy na maandishi katika pete.

Balozi wa Iran nchini Malaysia Ali Asghar Mohammadi na Mwambata wa Utamaduni Mohammad Oraei Karimi waliandamana na afisa huyo mkuu wa Malaysia katika ziara hiyo.

Tamasha la Kimataifa la Sanaa la Qur'ani la Restu linafanyika Januari 20 hadi 29 huko Putrajaya, Malaysia.

Hafla hiyo imeandaliwa na taasisi nyingi za Malaysia ikiwa ni pamoja na Wakfu wa Restu na washirika wa kigeni kama vile kituo cha kitamaduni cha Iran huko Malaysia na inafanyika katika Nasyrul Quran Complex huko Putrajaya.

Kulingana na kitabu cha programu kilichotolewa na waandaaji, hafla hiyo inawaruhusu wageni kushuhudia maonyesho maalum, na kuingiliana na wajasiriamali katika sekta za Qur'ani Tukufu na sanaa ya Kiislamu na bidhaa za Kiislamu huku pia wakijaribu kuboresha taswira ya Uislamu kama dini iliyojumuisha na ya amani.

Kuanzisha uhifadhi na ustawi wa Qur'ani Tukufu, kutukuza mafundisho ya Uislamu, kualika umma kupenda elimu na wanazuoni, kutumia teknolojia ya kisasa kama njia ya kuhubiri yenye ufanisi, na kujaribu kurudisha umma wa Kiislamu kwenye utambulisho wao wa kweli yametajwa miongoni mwa malengo mengine ya tamasha hilo.

Iran pia imetuma ujumbe, wakiwemo wasanii, kwenye hafla hiyo ili kutambulisha mafanikio na sera zake za Qur'ani pamoja na teknolojia mpya za Qur'ani.

.

 

4117800

captcha