Mohammad Al-Jundi alisema kuwa hivi karibuni baraza lilifanya uamuzi wa kupiga marufuku matumizi ya karatasi za rangi katika uchapishaji wa nakala za Qur'ani, likibainisha kuwa maandishi meusi ndiyo rangi pekee inayofaa kwa maandishi ya Qur'ani.
Aliongeza kuwa uamuzi huu ulifanyika kwa lengo la kuhifadhi heshima na hadhi ya Qur'ani Tukufu, na kwa hivyo, hakuna ruhusa zitakazotolewa kwa uchapishaji na uchapaji wa nakala za Qur'ani zenye rangi nchini Misri.
Alisema Kamati ya Mapitio ya Misahafu au Qur'ani Zilizochapishwa ina jukumu kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, akiongeza kuwa suala la kuhakikisha uchapaji sahihi wa Qur'ani, kwa mujibu wa mapitio na usimamizi, ni muhimu sana na kwa hivyo, baraza hilo linazingatia sana jambo hili.
Al-Jundi alieleza kuwa mapitio ya Qur'ani zinazochapishwa nchini Misri hufanywa na kikundi cha wataalam wa sayansi za Qur'ani, ambao ni wanachama wa kitivo cha Chuo cha Qur'ani cha Chuo Kikuu cha Al-Azhar na taasisi nyingine zinazobobea katika Qara’at za Qur'ani.
Inafaa kutajwa kuwa baraza hapo awali lilitoa amri ya kupiga marufuku uchapishaji wa nakala zaQur'ani kwa kutumia rangi za kung'aa na neon nchini Misri, likipinga uuzaji wa nakala hizi zenye rangi za Qur'ani kwenye soko la nchi hiyo.
Kwa mujibu wa miongozo ya baraza hilo, maandishi ya Qur'ani Tukufu yanapaswa tu kuandikwa kwa wino mweusi, kwenye kurasa nyeupe au ya rangi ya krimu.
Aidha, taasisi yoyote ya uchapishaji itakayoshindwa kufuata vigezo vilivyowekwa vya uchapishaji wa Qur'ani Tukufu, suala hilo litaripotiwa kwa mamlaka za utekelezaji, na nakala hizo zitaondolewa sokoni. Kwa kuongeza, taasisi ya uchapishaji iliyohusika itapokonywa haki ya kuchapisha Qur'ani.
349257