IQNA

Tanzania kuwakaribisha maqarii maarufu kutoka Iran katika hafla kubwa ya Qur’ani

16:04 - May 12, 2025
Habari ID: 3480676
IQNA – Maqari mashuhuri wa Qur'ani kutoka Iran wanatarajiwa kuzuru Tanzania kushiriki katika kongamano kubwa la kimataifa la Qur'ani litakalofanyika jijini Dar es Salaam.

Tukio hili la kimataifa lenye jina “Sauti ya Rehema” (Voice of Mercy) limepangwa kufanyika tarehe 25 Mei 2025  Dar es Salaam, mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania, kulingana na bango rasmi lililosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mkutano huu mkubwa wa Qur’ani, ukiwa na kaulimbiu “Mkusanyiko Mkuu Katika Nuru ya Qur’ani”, utawakutanisha wasomaji mashuhuri wa Qur’ani kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Miongoni mwa wasomaji Qur'ani watakaoshiriki ni nyota wanaotambulika kimataifa kama vile Hamed Shakernejad na Ahmad Abolghasemi kutoka Iran. Wawili hao ni miongoni mwa wasomaji mashuhuri wa Qur’ani kutoka Iran na ni waongozaji wa kipindi maarufu cha  Mahfel kanali ya 3 ya televisheni ya Iran , ambacho kimepata watazamaji wengi duniani. Hivi karibuni, maqari hao wawili walishiriki katika mijumuiko mkiubwa ya Qur’ani nchini Indonesia.

Maqari wengine waliothibitishwa kushiriki ni Sayed Jalal Masoomi, pia kutoka kipindi cha Mahfel TV, na maqari wawili mashuhuri wa Tanzania ambao Rajai Ayoub na Iddi Shaaban.

Vilevile, vijana wawili kutoka Iran, Mohammad Hossein Azimi na Mohanna Ghanbari, nao pia watasoma Qur’ani katika hafla hiyo.

Tukio hilo litatifanyika katika Uwanja wa Mnazi Mmoja na litaanza saa 3:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni kwa saa za Tanzania.

Tukio hili linaungwa mkono na taasisi mbalimbali za kidini na kitamaduni, ikiwa ni pamoja na Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Tanzania, BAKWATA (Baraza Kuu la Waislamu Tanzania), na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa.

3493042

captcha