IQNA

Jinai za Israel

Idadi ya waliouawa Gaza yazidi 42,000, Erdogan asema Israel ni 'Shirika la Kigaidi la Kizayuni'

12:38 - October 10, 2024
Habari ID: 3479569
IQNA - Idadi ya Wapalestina waliouawa kwa mabomu na risasi za Israel katika Ukanda wa Gaza tokea Oktoba mwaka jana sasa imepindukia 42,000, wengi wakiwa ni wanawake na watoto.

Idadi ya waliouawa Gaza yazidi 42,000, Erdogan asema Israel ni 'Shirika la Kigaidi la Kizayuni'Takriban Wapalestina 45 zaidi waliuawa katika mashambulizi ya jeshi katili la Israel katika Ukanda wa Gaza, na kufanya jumla ya vifo tangu Oktoba mwaka kupindukia  42,010, Wizara ya Afya katika eneo hilo ilisema Jumatano.

Taarifa ya wizara hiyo iliongeza kuwa wengine 97,720 walijeruhiwa katika mauaji ya kimbari yanayoendelea kutekeleza na utawala dhalimu wa Israel dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo.

Wakati huo huo, Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amekosoa vikali mashambulio ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon na Gaza na kuitaja Israel kuwa ni "shirika la kigaidi la Kizayuni".

Erdogan ambaye alikuwa akizungumza mbele ya wabunge wa chama tawala cha Uadilifu na Maendeleo (Adalet ve Kalkınma Partisi-AKP) , kwa mara nyingine tena amekosoa madola ya Magharibi hasa Marekani kutokana na hatua yao kuunga mkono utawala katili wa Israel.

3490209

Rais wa Uturuki pia ameonya kwamba mzozo kati ya Iran na Israel umeongeza hatari ya vita vya kikanda.

Erdogan hapo awali alimwita Benjamin Netanyahu "mchinjaji wa Gaza" na kumlinganisha yeye na serikali yake na Hitler na serikali ya Ujerumani ya Nazi.

Habari zinazohusiana
captcha