IQNA

Kitabu kipya chafafanua historia ya zana z kuandika Qur’ani

17:39 - July 16, 2025
Habari ID: 3480955
IQNA – Taasisi ya Mfalme Abdulaziz nchini Saudi Arabia imechapisha kitabu kipya kwa lugha ya Kiarabu kinachofuatilia historia ya maendeleo ya zana zilizotumika kuandika Qur’ani Tukufu.

Kitabu hicho cha kitaaluma, chenye kurasa 172, kimeandikwa na Abdulmohsen bin Mohammed bin Muammar, kikibeba jina “Zana za Kuandika Qur’ani Katika Historia”. Kinachunguza mabadiliko ya vifaa vilivyotumika kuandika Qur’ani tangu wakati wa Wahy hadi zama za uchapishaji wa kisasa wa kidijitali.

Kwa mujibu wa elmstba.net, kitabu hiki kinatoa muhtasari wa kihistoria kuhusu jinsi Waislamu walivyohifadhi na kunakili Qur’ani kwa zaidi ya karne kumi na nne.

Kinaanza kwa kuelezea mbinu za awali za kuandika wakati wa Mtume Muhammad (SAW), kama vile matumizi ya ngozi, vibao vya mbao, na mawe.

Mwandishi anachambua hatua muhimu za kihistoria, ikiwemo ukusanyaji wa Qur’ani wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr  na uidhinishaji wa maandiko chini ya Khalifa Uthman ibn Affan.  Maendeleo ya baadaye kama vile kuongezwa kwa alama za matamshi, mapambo ya maandishi, na matumizi ya karatasi, kurekodi kwa sauti, na teknolojia ya uchapishaji wa kidijitali pia yameangaziwa.

Moja ya sifa za kipekee za kitabu hiki ni ujumuishaji wa picha adimu zinazoonyesha mifano halisi ya zana za kihistoria za kuandika—kutoka kalamu na wino hadi ngozi, mbao na karatasi—na hivyo kuwapa wasomaji kile mwandishi anakielezea kama “uzoefu wa kipekee wa kuona uliothibitishwa kisayansi.”

Kitabu pia kinajadili sifa na tofauti za vifaa mbalimbali vya kuandika, na kuwataja Maswahaba wa Mtume (SAW) waliokuwa wakinakili wahyi.

4294505

captcha