Kulingana na Idara ya Waqf ya Kiislamu, Sala za Isha na Taraweeh ziliswaliwa licha ya hatua kali za kijeshi zilizowekwa na mamlaka za utawala wa Israel, ambazo zimezuia waumini wengi kufika katika eneo hilo takatifu.
Idara ya Waqf ya Kiislamu ilibainisha kuwa wengi wa waumini walikuwa wakazi wa al-Quds.
Hata hivyo, utawala dhalimu wa Israel uliwazuia maelfu ya Wapalestina kutoka Ukingo wa Magharibi kufika msikitini ili kushiriki katika sala hizo.
Vyanzo vya ndani viliongeza kuwa vikosi vya Israel viliongeza ukaguzi wa usalama katika maeneo muhimu ya kuingilia, ikiwa ni pamoja na Lango la Damascus na Lango la Simba, ambapo walikagua vitambulisho vya waumini. Vijana kadhaa wa Kipalestina waliripotiwa kukamatwa na kunyimwa kuingia katika eneo hilo.
Msikiti wa Al-Aqsa, moja ya maeneo matakatifu zaidi katika Uislamu, kwa kawaida hushuhudia idadi kubwa ya Wapalestina wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kwa hofu ya mkusanyiko mkubwa wa Waislamu, vikosi vya utawala wa Kizayuni wa Israeli mara nyingi huweka vikwazo vya kufika katika msikiti huo.
3492115