IQNA

Uwanja wa Ben Gurion wafungwa tena kufuatia shambulio la kombora la Yemen

15:18 - July 07, 2025
Habari ID: 3480912
IQNA- Mamlaka ya anga ya Israel imesitisha safari zote za ndege za kuwasili na kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ben Gurion na kusema kuwa kituo hicho kitaendelea kufungwa "kwa muda usiojulikana" baada ya Vikosi vya Wanajeshi wa Yemen kufanya shambulio la kombora, kulipiza kisasi vita vya mauaji ya halaiki vinavyoendelea vya utawala wa Tel Aviv dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Vyombo vya habari vya Kiarabu vimeripoti kuwa, maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel yalikatishwa na safari za anga za kimataifa mapema leo Jumapili, huku ving'ora vya tahadhari vikihanikiza katika maeneo mengi katika eneo la Bahari ya Chumvi (Bahari Maiti) kufuatia kuvurumishwa kwa kombora la balestiki. Hakukuwa na ripoti za majeraha au uharibifu.

Jeshi la Israel baadaye lilidai katika taarifa fupi kwamba, mifumo yake ya kutungua makombora eti imefanikiwa kulitungua kombora hilo la balestiki la Yemen.

Hatua hiyo imekuja chini ya wiki moja baada ya jeshi la Yemen kukiri kuhusika na kurusha kombora la balestiki lililolenga uwanja huo wa ndege wa Ben Gurion.

Katika taarifa ya televisheni iliyotangazwa na al-Masirah TV mnamo Julai 1, msemaji wa jeshi la Yemen Brigedia Jenerali Yahya Saree alisema "wameendesha operesheni maalum ya kijeshi kwa kulenga uwanja wa ndege wa Ben Gurion huko Tel Aviv kwa kutumia kombora la balestiki aina ya Palestina-2."

Aliongeza kuwa, shambulio hilo la makombora "limefikia lengo lake" kwa kulazimisha "mamilioni ya walowezi kwenye makazi yanayokaliwa kwa mabavu kukatiza safari zao katika uwanja huo wa ndege."

Aidha Saree amesema kuwa wimbi la mashambulizi ya wa vikosi vya Yemen kwa kutumia ndege zisizo na rubani (UAV) yalilenga "maeneo matatu nyeti" huko Eilat, Tel Aviv, na Ashkelon.

3493731

Habari zinazohusiana
captcha