IQNA

Mufti wa New Zealand apongeza hafla ya Saa ya Qur’ans nchini Malaysia

17:44 - August 31, 2025
Habari ID: 3481165
IQNA – Mufti wa New Zealand ameipongeza hafla ya Malaysia 'Quran Hour' yaani Saa ya Qur'ani kwa kuhamasisha Waislamu kuhusu Kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu.

Mfululizo wa Malaysia wa  #QuranHour, ambao sasa umefikia mwaka wake wa 11, unaendelea kuonyesha njia yake ya kipekee ya kuwahamasisha watu kupenda na kufungamana na Qur’ani Tukufu.

Mufti wa New Zealand, Sheikh Mohammad Amir, alishiriki kwa mara ya kwanza katika programu hii mwaka huu na alitaja mtiririko wa tukio la saa moja kama wa kipekee na wa kufana.

Alisema kwamba kikao alichoshiriki kilikuwa na qiraa Qur’an kutoka kwa maqari mbalimbali, kilichojumuishwa na tafsiri za maana, kilichowafanya washiriki kuwa makini na kushiriki kikamilifu.

“Programu hii kuwa ni ya kuvutia sana na ina uwezo wa kukua zaidi huku ikiendelea kuongeza uelewa miongoni mwa Waislamu kuhusu Qur’ani. Wanaweza kujihisi na kutafakari kuhusu nafsi zao wakati wanapojifunza kila aya ya kitabu hiki kitakatifu ili kujitayarisha kwa ajili ya akhera, Insha’Allah.”

“Bila shaka, nitajivunia na kupata fahari kama programu hii ingeweza kuanzishwa duniani kote, ikiwa ni pamoja na New Zealand, siku moja,” alisema alipokutana na waandishi wa habari baada ya tukio hilo lililofanyika kwenye Msikiti Mkuu wa Kitaifa wa Kuala Lumpur, Jumamosi.

Programu hiyo pia ilihudhuriwa na Naibu Waziri Mkuu wa Malaysia, Ahmad Zahid Hamidi, Waziri katika Idara ya Waziri Mkuu (Masuala ya Kidini), Mohd Na’im Mokhtar, na Mufti wa Maeneo ya Shirikisho, Ahmad Fauwaz Fadzil.

Viongozi wa kidiplomasia kutoka nje walikuwapo miongoni mwa wageni, wakiwemo Balozi wa Senegal, Abdoulaye Barro, Balozi wa Uturuki, Emir Salim Yuksel, Balozi wa Yordani, Dr. Ismael Maaytah, na Balozi wa Misri, Karim Mohamed Elsadat Abdelkarim.

Waandaaji wa Malaysia #QuranHour 2025, Mwasisi wa Warisan Ummah Ikhlas Foundation (WUIF), Hussamuddin Yaacub, na Mkurugenzi Mtendaji wa WUIF, Marhaini Yusoff, walihudhuria pia.

Akirejelea uzoefu wake nchini Malaysia, Sheikh Mohammad Amir alibaini kuwa nchi hii inatambulika sana kwa matukio yake ya kidini, ambayo yanaweza pia kuenezwa kama sehemu ya utalii wa Kiislamu.

“Nimekuwa Malaysia mara nyingi kushiriki mihadhara na mikutano. Nchi hii inatambulika kwa programu mbalimbali za kidini. Kuna mambo mengi mazuri ya kupatikana hapa Malaysia pia, na sisi kama wageni kutoka nje, kila wakati tunaona kwamba nchi hii ni bora na inatoa faida nyingi,” aliongeza.

3494432

captcha