Mashindano haya yalihusisha kipengele cha kuhifadhi Qur’ani yote kwa jumla. Washindi walitangazwa na kutunukiwa zawadi katika hafla ya kufunga mashindano hayo siku ya Alhamisi.
Jopo la majaji lilimtangaza mshiriki kutoka Saudi Arabia kuwa mshindi wa kwanza. Mshiriki kutoka Tajikistan alishika nafasi ya pili, huku mwakilishi wa nchi mwenyeji, Kazakhstan, akichukua nafasi ya tatu. Washiriki kutoka Urusi na Misri walishika nafasi ya nne na tano mtawalia.
Mashindano haya yaliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mambo ya Kiislamu ya Saudi Arabia na Mamlaka ya Kiroho ya Waislamu wa Kazakhstan. Tukio hili liliwaleta pamoja washiriki 22 kutoka nchi 21, zikiwemo Iran, Saudi Arabia, Kazakhstan, Bahrain, Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri, Palestina, Morocco, Algeria, Jordan, Uturuki, Malaysia, Pakistan, Kyrgyzstan, Jamhuri ya Azerbaijan, Indonesia, Tajikistan, Uzbekistan, na Urusi.
Mashindano haya yalifanyika kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Jamhuri ya Kazakhstan na kumbukumbu ya miaka 35 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kiroho wa Waislamu wa Kazakhstan.
4311257