IQNA

Qurani

Wairani wanne washiriki Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iraq

15:59 - November 09, 2024
Habari ID: 3479722
IQNA - Kuna wanaharakati wanne wa Qur'ani wa Iran wanaohudhuria mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iraq yaliyoanza mjini Baghdad siku ya Jumamosi.

Wawili kati yao ni washindani huku wengine wawili wakihudumu katika jopo la majaji.
Jumla ya washiriki 31 kutoka nchi kadhaa wanashiriki katika mashindano hayo yanayojulikana rasmi kama Tuzo la Kimataifa la Qur'ani la Iraq.
Mashindano hayo yameandaliwa na Kituo cha Kitaifa cha Sayansi ya Qur'ani nchini Iraq kwa ushirikiano na mashirika ya Wakfu  ya Shia na Sunni chini ya kauli mbiu ya, “Kutoka Baghdad, Nembo ya Ustaarabu na Uislamu, hadi Gaza, Nembo ya Muqawama, na Lebanoni, Nembo ya Jihadi; Kupitia Qur’ani, Tunapata Ushindi na Uthabiti.”
Mehdi Shayeq anaiwakilisha Iran katika kitengo cha usomaji wa Qur'ani huku Ali Gholamazad akishindana katika kuhifadhi Qur'ani nzima.
Wataalamu wa Qur'ani Qassem Raziei na Mutaz Aghaei ni wajumbe wa Iran katika jopo la majaji.
Shayegh, 36, anatoka katikati mwa jiji la Yazd. Ameshinda tuzo kadhaa katika matukio ya kimataifa ya Qur'ani, ikiwa ni pamoja na nafasi  kwanza katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tunisia.
Gholamazad mwenye umri wa miaka 24, ambaye anatoka mji wa kaskazini wa Zanjan, alishika nafasi ya tatu katika toleo la 39 la mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Kroatia.

3490619

captcha