Tukio hilo lililotokea lilifikishwa kwa maafisa wa chuo hicho Alhamisi iliyopita, gazeti la The Chronicle liliripoti Jumatatu.
Aya ya Qur'ani Tukufu kwenye bango hilo , inayosomeka "Mola wetu, hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu," ilibadilishwa na kuingiza neno "si" kabla ya "Mwenye kurehemu."
Maafisa wakuu wa chuo hicho walisisitiza kuwa upotoshaji huo wa aya hiyo unaweza kuwakera sana Waislamu na kuchangia katika dhana potofu zenye madhara zinazoweza kuchochea ghasia dhidi ya umma wa Kiislamu.
Zaidi ya hayo, taarifa hiyo ilizungumzia kitendo cha pili cha uharibifu unaohusisha mabango ya ng'ombe wekundu.
Taswira ya ng'ombe huyo mwekundu inahusishwa na matamshi ya itikadi kali ya Kiyahudi ya kutetea mpango wa kubomoa wa msikiti wa al-Aqswa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.
Mashirika ya haki za binadamu yamelinganisha kuenea chuki dhidi ya Uislamu baada ya operesheni ya kimbunga cha al-Aqsa mnamo Oktoba 7 na tuhuma dhidi ya Waislamu baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001 nchini Marekani. Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu (CAIR) limetangaza kuwa katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho ya 2023, malalamiko 578 kuhusu chuki dhidi ya Waislamu na Wapalestina yaliripotiwa. Idadi hiyo iliongezeka kwa asilimia 178 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliotangulia.
3488132