IQNA

Jinai za Israel

CAIR: Israel imefuta familia 902 huko Gaza na hilo ni thibitisho la mauaji ya kimbari

22:01 - October 06, 2024
Habari ID: 3479549
IQNA – Ukweli kwamba utawala haramu wa Israel umeangamiza familia 902 katika Ukanda wa Gaza katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ni ushahidi usiopingika wa dhamira ya utawala wa Israel kutekeleza mauaji ya kimbari.

Haya ni kwa mujibu wa Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani (CAIR), shirika kubwa zaidi la kutetea haki za Waislamu wa Marekani na utetezi.
Jeshi la utawala ghasibu wa Israel limeripotiwa kuzifuta familia 902 za Wapalestina katika sajili ya kiraia katika Ukanda wa Gaza tangu Oktoba mwaka jana.
 Katika taarifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taifa wa CAIR Nihad Awad alisema:
"Kufutwa kabisa kwa zaidi ya familia 900 ni uthibitisho usiopingika wa dhamira ya utawala wa mrengo wa kulia w Israel wa mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina huko Gaza. Ukatili huu hauwezi kupuuzwa, na hauwezi kusamehewa. Utawala wa Biden lazima uache kuunga mkono mauaji ya jumla ya familia na kulazimisha utawala wa Israel kusitisha kampeni yake ya mauaji ya kimbari.”
Amebaini kuwa, CAIR ilisema utawala wa Biden lazima ukomeshe mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza na yasirudiwe tena katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu baada ya shambulio la anga la Israel kwenye mgahawa katika kambi ya wakimbizi ya Tulkarem kuwauwa Wapalestina 18 na kuwajeruhi wengine wengi.”
Utawala wa Israel umeendeleza vita vyake vya mauaji ya kimbari  dhidi ya Gaza tangu Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas,  lilipotekeleza operesheni ya kulipiza kisasi jinai za miongo kadhaa za Israel Oktoba 7 mwaka jana..
Takriban watu 42,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wameuawa na zaidi ya 95,000 kujeruhiwa katika mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza.
Mashambulizi hayo ya Israel yamewafanya takriban wakazi wote wa eneo hilo kuwa wakimbizi kutokana na mzingiro unaoendelea ambao umesababisha uhaba mkubwa wa chakula, maji safi na dawa.
Israel inakabiliwa na tuhuma za mauaji ya halaiki kwa vitendo vyake huko Gaza katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).

3490154

 

Habari zinazohusiana
captcha