Kanda za video zilizosambazwa na shirika la uokoaji kwenye chaneli yake ya Telegram mnamo Ijumaa zilionyesha wafanyikazi wakiwavuta waathiriwa kutoka kwa uchafu wa nyumba ya familia huko Jabalia. Mahmoud Basal, msemaji wa shirika hilo, alithibitisha kwa AFP kwamba uvamizi huo wa anga ulijeruhi watu wengine 15.
Watoto hao walisemekana kuwa na umri wa miaka sita na chini.
Mashambulizi ya anga yaliendelea kote Gaza siku ya Ijumaa, na kuendeleza mashambulizi ambayo yameendelea kwa zaidi ya miezi 14.
Katika tukio tofauti, watu wanane waliuawa katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat wakati jengo la makazi lilipopigwa na kombora la ndege isiyo na rubani, kulingana na Hospitali ya Mashahidi wa Al-Aqsa.
Zaidi ya hayo, watu wanne, wakiwemo wasichana wawili na wazazi wao, walipoteza maisha huko Beit Hanoon kufuatia uvamizi mwingine wa anga uliotekelezwa na jehi katili la Israel.
Vikosi vya uokoaji pia viliopoa miili ya ndugu watatu kutoka kwenye magofu ya nyumba iliyolipuliwa karibu na Hospitali ya Kamal Adwan.
Hali mbaya ya kibinadamu huko Gaza ilisababisha onyo kutoka kwa Louise Waterridge, Afisa Mwandamizi wa Dharura wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi (UNRWA).
Akizungumza kutoka kambi ya Nuseirat, alielezea Gaza kama "makaburi," na zaidi ya wakazi milioni mbili wamekwama katika hali mbaya.
"Watu wengi wanaishi katika hema, bila makazi sahihi," Waterridge alisema. "Pamoja na asilimia 69 ya majengo kuharibiwa au kubomolewa, familia hazina mahali kujikinda na baridhi kali. Haiwezekani kujikinga katika hali hizi."
Tangu Oktoba 7, 2023, wakati Israel, kwa msaada wa Marekani, ilipoanzisha mashambulizi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza, mashambulizi hao yamesababisha vifo vya Wapalestina 45,206 na kujeruhi 107,512 wengi wakiwa ni wanawake na watoto.
3491138