IQNA

Mwanazuoni wa Kisunni wa Pakistan: Iran imeshinda vita visivyo na usawa dhidi ya Marekani na Israel

22:13 - March 11, 2026
Habari ID: 3482045
IQNA-Mwanazuoni mashuhuri wa Ahlus-Sunna nchini Pakistan ametaja kwa sifa kubwa ubora wa kijeshi na kiuwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, licha ya kupita siku 11 tangu kuanza kwa uvamizi wa kijeshi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel. Amesema: Wavamizi bado wako katika ndoto ya ushindi, lakini Iran imevunja kiburi cha bandia cha ngome za Marekani na Israel.

Kwa mujibu wa taarifa ya IQNA kutoka vyombo vya habari vya Pakistan, Mufi Muneebur Rahman, Mkuu wa Chuo cha Kiislamu Jamia Naeemia na pia Rais wa Jumuiya ya Vyuo vya Kisunni Pakistan, katika tamko alilolitoa ameitetea Iran kwa hatua zake za ulinzi dhidi ya uhasama wa Marekani na utawala wa Kizayuni, na kwa kulenga maslahi yao ya kijeshi katika eneo.

Amesema: Trump anaonyesha kana kwamba yeye ndiye mshindi wa uwanja wa vita, na dunia inaonekana kucheza kwa ala yake, lakini ukweli uko wazi kama mwanga wa mchana – Iran imevunja mamlaka ya bandia ya Marekani na Israel.

Mufi huyo wa Kisunni aliongeza: Sasa zimepita siku kumi na moja tangu kuanza kwa vita vilivyochochewa na Marekani na utawala wa Kizayuni, lakini wavamizi bado wanaota ndoto za ushindi. Uwezo wa uwanja wa vita na nguvu ya kiakili ni upande wa Iran.

Amefafanua: Iran, licha ya vikwazo vya Marekani vilivyodumu kwa miaka 47 ambavyo vimeathiri uchumi na uwezo wa kijeshi, imeweza kusimama imara katika vita visivyo na uwiano na haijanyenyekea kwa matakwa ya Marekani.

Mufi Muneebur Rahman ameendelea kusema kuwa: Marekani inadai kuwa eti imeshinda. Madai hayo hayana msingi wala uhalali; dunia nzima inaitambua Iran kama mshindi halisi wa vita, kwa sababu licha ya hasara ya kifedha na kiuchumi, taifa hilo limebaki likiwa na moyo wa ujasiri na uthabiti.

Uvamizi wa Kijeshi wa Marekani na Israel Dhidi ya Iran

Uvamizi wa kijeshi wa pamoja wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulianza alfajiri ya tarehe 10 Ramadhani sawa na Februari 28, 2026. Katika saa za awali za uvamizi huo wa kigaidi, Ayatullah Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, aliuawa shahidi akiwa katika kikao na makamanda wa kijeshi ndani ya ofisi yake. Uvamizi huo umejiri wakati mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani, kwa upatanishi wa Oman, yalikuwa yanaendelea.

Wachambuzi wamesema kuwa jambo hilo limedhihirisha kwamba Marekani kwa vitendo haizingatii misingi ya mazungumzo, uaminifu na suluhu ya amani, bali bado inategemea chaguo la kijeshi kama chombo cha shinikizo la kisiasa.

Jibu la Iran

Baada ya kuanza kwa uvamizi huo wa pamoja, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaendelea kutoa jibu la kuthibitisha haki yake, lenye ukali, uangalifu na uwiano na kitendo hicho cha uhasama.

Majeshi ya Iran yamelenga ngome za kijeshi, kijasusi na kisiasa za utawala wa Kizayuni katika, pamoja na ngome na vituo vya wanajeshi wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi. Hatua za kulipiza kisasi ambazo Iran imechukua ni kwa mujibu wa sheria na kanuni za kimataifa za kujilinda na kukabiliana na wavamizi.

4339941

Kishikizo: shahidi imam khamenei
captcha