IQNA

Nujaba: Mapambano ya sasa ni Mvutano kati ya Nguvu za Ukafiri na Mhihimili wa Heshima na Utukufu

16:06 - March 17, 2026
Habari ID: 3482066
IQNA – Msemaji wa harakati ya muqawama ya Iraq, al‑Nujaba, ameeleza mapambano yanayoendelea katika eneo la Asia Magharii kuwa ni mvutano kati ya nguvu za ukafiri na mhimili wa heshima na utukufu.

Hussein al‑Moussawi alitoa kauli hiyo wakati wa kile alichokitaja kuwa ni uchokozi unaoendelea wa Marekani na Israel dhidi ya Iran, Lebanon na Iraq.

Akirejelea damu iliyomwagika nchini Iraq na msimamo usioridhisha wa serikali katika kukabiliana na changamoto zinazokaribia, alisisitiza kwamba Iraq, bila kujali shinikizo lolote la nje, haitawahi kuafikiana kwa kuyasaliti maadili yake halisi ya Kiislamu wala misingi yake ya kitaifa.

Al‑Moussawi ameikosoa vikali serikali ya Iraq kwa ukimya na udhaifu wake mbele ya vitisho vinavyoongezeka dhidi ya nchi hiyo na eneo kwa ujumla, akisema kuwa mtazamo huo haulingani na hatari ya hali ya sasa.

Aidha ameushutumu utawala  Kizayuni na Marekani kwa kulisukuma eneo hilo katika hali hatarishi.

Msemaji wa al‑Nujaba amesema kuwa mapambano ya sasa ni mvutano kati ya nguvu za ukafiri na mhimili wa heshima na utukufu, akisisitiza kwamba Iraq itaendelea kushikamana kikamilifu na misingi yake.

Pia alikataa mantiki ya vitisho na akatoa wito wa kuchukuliwa msimamo thabiti na wenye heshima katika kukabiliana na changamoto hizi.

3496793

captcha