
Ayatullah Seyyed Mojtaba Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameshukuru na kuwapongeza wanazuoni wakuu wa kidini na wananchi wa Iraq kwa misimamo yao ya wazi dhidi ya uvamizi na uchokozi wa maadui wa Iran.
Kufuatia wito wa Ayatollah Ali Sistani, Marja Mkuu wa Waislamu wa Iraq, kwa ajili ya kuisaidia Iran, msafara wa kwanza wa misaada ya umma umeondoka katika Haram Tukufu ya Imam Hussein (as) katika mji mtakatifu wa Karabala kuelekea Iran.
Awali, Ofisi ya Marja Mkuu huyo wa Iraq ililaani kwa maneno makali vita vya kieneo dhidi ya Iran na kuwataka Waislamu wote na watu huru duniani kuvilaani na kuonyesha mshikamano na mataifa madhulumu ya Iran na Lebanon.
Marekani na utawala haramu wa Israel zimekuwa zikiendesha mashambulio makali ya kichokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tangu tarehe 28 Februari, ambapo zimelenga na kuwaua kigaidi watoto wadogo wakiwa shuleni, viongozi wa ngazi za juu serikalini na pia kuharibu kiholela miundombinu ya nchi vikiwemo vituo vya kuzalisha umeme, nishati na pia vyuo vikuu.
3496920