Khatma ya Qur’ani inamaanisha kusoma Qur’ani Tukufu kuanzia mwanzo hadi mwisho wake au Kuhitimisha Qur’ani.
Wissam Nazir Al‑Dulfi, mkuu wa Kituo cha Habari za Qur’ani katika Idara ya Mfawidhi wa Haram Tukufu, alisema kuwa kutokana na juhudi za pamoja za maafisa wa Kitengo cha Shughuli za Qur’ani kwa Njia ya Mtandaoni, idadi ya khatma za Qur’ani zilizofanyika katika mazingira ya mtandao imefikia 1,605.
Alisema programu hii ilifanyika kutokana na juhudi za Muhammad Al‑Tai, mkuu wa Kitengo cha Shughuli za Qur’ani kwa Njia ya Mtandaoni, kwa uratibu wa Umm Eilaf Al‑Halfi na chini ya usimamizi wa Murtaza Jamal Al‑Din, mkuu wa idara ya taaluma.
Al‑Dulfi aliongeza kuwa walimu wanawake wa Qur’ani wamekuwa na mchango mkubwa katika kuendesha khatma hizi za Qur’ani, ambapo walimu wanawake 284 kutoka shule 9 za Qur’ani za mtandaoni wameshiriki katika programu hiyo.
Kuhusu namna khatma hizo zilivyopangwa, alisema kuwa walimu pamoja na wanafunzi wa hifdh ya Qur’ani wameshiriki katika programu hiyo kwa njia ya mtandao kwa utaratibu maalumu, wakisoma Qur’ani kwa kufuata ratiba iliyopangwa mapema.
Al‑Dulfi pia alibainisha kwamba mbali na khatma za Qur’ani, kuna programu ya kielimu inayotekelezwa kupitia Telegram, inayojumuisha mawasiliano ya moja kwa moja na wanafunzi wa Qur’ani, huku kila shule ikiwa na idadi maalumu ya washiriki.
3496993