malaysia - Ukurasa 2

IQNA

IQNA – Kifaa kipya cha kielektroniki cha eBraille kilichotengenezwa nchini Malaysia kimeleta mageuzi makubwa katika kujifunza Qur'ani Tukufu kwa watu wenye uoni hafifu, au ulemavu wa macho kwa kuwapa uwezo wa kupata maandiko ya dini moja kwa moja kwa njia ambayo haijawahi kupatikana hapo awali, sambamba na kufungua fursa katika nyanja nyingine za elimu.
Habari ID: 3481789   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/11

IQNA – Imamu wa Msikiti wa Al-Aqsa amesifu msaada wa Malaysia kwa Palestina na kulaani ukatili wa Israel dhidi ya Wapalestina.
Habari ID: 3481776   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/06

IQNA – Malaysia imeanza kuchapisha nakala 20,000 za Qur’an Tukufu zikiwa na tarjuma ya Kitamil.
Habari ID: 3481687   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/20

IQNA – Mkutano wa Dunia wa Qur’ani 2025 umefunguliwa Jumapili jijini Kuala Lumpur kwa wito mkali kwa viongozi wa Kiislamu na jamii kugeuza thamani za Qur’ani kuwa mikakati halisi ya kijamii na kiuchumi, ukisisitiza nafasi ya Kitabu Kitukufu kama mwongozo wa vitendo katika utungaji sera na utatuzi wa changamoto za kisasa.
Habari ID: 3481625   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/07

IQNA – Kitabu kipya chenye tafakuri fupi 365 za kila siku kuhusu Qur’ani kimezinduliwa mjini Petaling Jaya, Malaysia, siku ya Ijumaa.
Habari ID: 3481621   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/06

IQNA – Mkutano wa Dunia wa Qur’ani 2025 ukifunguliwa Kuala Lumpur mwishoni mwa wiki hii, ukitoa jukwaa la mazungumzo kati ya ujuzi wa kielimu wa kiroho na vitendo vya kiviwanda.
Habari ID: 3481611   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/03

IQNA – Serikali ya Malaysia imezindua mfumo mpya uitwao iTAQ unaotumia teknolojia ya Akili Mnemba (AI) kuharakisha mchakato wa kuthibitisha usahihi wa machapisho ya nakala za Qur'ani Tukufu.
Habari ID: 3481441   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/31

IQNA – Mwanazuoni na mwanaharakati kutoka Malaysia ametoa wito kwa Waislamu kote duniani kuonesha mshikamano kwa vitendo badala ya maneno, akisisitiza kuwa Qibla ya pamoja inapaswa kuwa msingi wa mshikamano wa Ummah.
Habari ID: 3481275   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/23

IQNA – Mwanaharakati kutoka Malaysia amesema kuwa mataifa ya Kiislamu yanapaswa kuangazia mambo yanayowafungamanisha na kushikamana kukabiliana na changamoto za pamoja.
Habari ID: 3481257   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/20

IQNA- Waislamu wa jimbo la Kedah nchini Malaysia wamepata fursa adhimu ya kubadilisha nakala zao za Qur'anI zilizochakaa au kuharibika kwa nakala mpya zilizoidhinishwa rasmi na Wizara ya Mambo ya Ndani bila malipo.
Habari ID: 3481194   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/07

IQNA – Maqari wakongwe wa Qur’ani kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) wamepongezwa kwa mafanikio yao katika Jukwaa la Kimataifa la Uhakiki wa Ijazah za Qur’ani na Kuheshimu Maqari wa ASEAN, lililofanyika nchini Malaysia.
Habari ID: 3481180   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/03

IQNA – Mufti wa New Zealand ameipongeza hafla ya Malaysia 'Quran Hour' yaani Saa ya Qur'ani kwa kuhamasisha Waislamu kuhusu Kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu.
Habari ID: 3481165   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/31

IQNA-Ujumbe wa viongozi wa kidini kutoka Iran, wakiongozwa na Ayatullah Alireza Arafi na Ayatullah Ahmad Mobaleghi, umefanya ziara ya siku tatu nchini Malaysia kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya muda mrefu ya kielimu na kidini kati ya mataifa hayo mawili.
Habari ID: 3481159   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/30

IQNA – Jimbo la Sarawak, Malaysia limeanzisha mbinu rafiki kwa mazingira katika kuheshimu na kuondosha nakala zilizochakaa za Misahafu au Qur’an Tukufu.
Habari ID: 3481094   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/16

IQNA – Mtaalamu wa Qur’ani kutoka Iran, Gholam Reza Shahmiveh, amepongeza historia ndefu ya Malaysia katika kuandaa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani, akiyataja kama mfano wa kitaalamu na utambulisho wa kitamaduni.
Habari ID: 3481092   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/16

IQNA – Qari bora wa kiume wa Malaysia katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani mwaka huu nchini humo amesema kuwa kujifunza kutoka kwa mashaikh wa qiraa’ah kutoka pembe zote za dunia kumemuwezesha kufikia ushindi huu.
Habari ID: 3481063   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/10

IQNA – Wawakilishi wawili kutoka Malaysia wametwaa ubingwa katika Mashindano ya 65 ya Kimataifa ya Kusoma na kuhifadhi Qur’ani Tukufu ya Malaysia (MTHQA) ya 65, kila mmoja katika kipengele chake husika.
Habari ID: 3481061   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/10

IQNA – Waziri Mkuu wa Malaysia amesema kuwa serikali yake itatenga ufadhili wa ziada kwa Yayasan Restu ili kuwezesha tafsiri ya Qur’ani Tukufu katika lugha nyengine 30, na hivyo kupanua zaidi upeo wa ujumbe wake wa ulimwengu.
Habari ID: 3481060   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/09

IQNA – Mashindano ya 65 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Malaysia (MTHQA), yameimarika kwa mtazamo wa viwango ambapo majaji wamepongeza mahadhi na uhifadhi ulio bora zaidi.
Habari ID: 3481056   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/09

IQNA – Katika ufunguzi wa Kongamano la Dunia la Qur’ani 2025 jijini Kuala Lumpur, Malaysia, wito umetolewa wa kuifanya Qur’ani kuwa mwongozo wa kina katika utungaji sera, elimu, na mikakati ya kiuchumi na isiwe ni ya usomaji na kuhifadhi pekee.
Habari ID: 3481052   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/09