TEHRAN (IQNA)- Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amebainisha wasiwasi wake juu ya kampeni ya utawala wa Israeli ya kuwakamata, kuwatesa na kuwakandamiza watetezi wa haki za binadamu wa Palestina kote Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
Habari ID: 3474187 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/13
TEHRAN (IQNA) - Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na walowezi wa Kizayuni walikiuka haki za Wapalestina katika zaidi ya mara 3,800 mwezi Julai katika katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na mjini al-Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3474162 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/05
TEHRAN (IQNA)- Maelfu ya waumini Wapalestina waslihisiri katika Sala ya Idul Adha iliyosaliwa katika Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) baada ya hujuma za siku kadhaa za Wazayuni dhidi ya Msikiti huo.
Habari ID: 3474117 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/22
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amelaani vikali hatua ya Marekani kuteka tovuti za vyombo vya habari vinavyounga mkono harakati za muqwama au mapambano ya Kiislamu na Iran katika eneo.
Habari ID: 3474074 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/06
TEHRAN (IQNA)- Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zimeshambulia maeneo ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika Ukanda wa Ghaza na hivyo kukiuka mapatano ya hivi karibuni ya usitishwaji vita.
Habari ID: 3474064 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/02
TEHRAN (IQNA)- Wazayuni wenye misimamo mikali wameuhujumu tena Msikiti wa al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) leo Jumatatu wakiwa chini ya himaya ya wanajeshi wa utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3474051 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/28
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah
TEHRAN (IQNA)- Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, vita vya Saif al Quds (Panga la Quds) vimepelekea kuwepo umoja na mshikamano wa muqawama kote Palestina.
Habari ID: 3473999 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/12
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika Ukanda wa Ghaza ametoa tamko baada ya kubainika kuwa Wazayuni wanapanga kutekeleza hujuma nyingine dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds au Jerusalem.
Habari ID: 3473983 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/06
TEHRAN (IQNA)- Walowezi wa Kizayuni, wakiwa wanalindwa na askari wa jeshi la utawala haramu wa Israel Jumatano waliuhujumu na kuuvunjia heshima Msikiti wa Al Aqsa katiak mji wa Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3473974 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/03
Kamanda wa Kikosi cha QUDS cha IRGC
TEHRAN (IQNA) - Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema wakati umefika kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kuanza kutafakari kuondoka katika ardhi za Palestina unaozikalia kwa mabavu haraka iwezekanavyo.
Habari ID: 3473962 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/30
TEHRAN (IQNA)- Sala ya Ijumaa imeswaliwa jana katika Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) ambapo inakadiriwa kuwa Wapalestina 40,000 walishiriki katika sala hiyo.
Habari ID: 3473959 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/29
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeutahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kufanya chokochoko na mashambulizi ya aina yoyote dhidi ya mji wa Quds (Jerusalem) na Msikiti Mtukufu wa al Aqsa mjini humo.
Habari ID: 3473942 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/24
TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Kenya jana waliandamana katika mji mkuu, Nairobi na kubainisha uungaji mkono wao kwa Wapalestina ambao wanakabiliwa na hujuma ya utawala wa Kizayuni wa Israel
Habari ID: 3473907 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/14
TEHRAN (IQNA)-Wapalestina karibu laki moja wameshiriki katika Sala ya Idul Fitr leo Alkhamisi asubuhi katika Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu katika mji wa Quds (Jerusalem) licha ya sheria kali zilizowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel ambao siku chache zilizopita wanajeshi wa utawala huo katili waliwashambulia kwa mabomu Waislamu waliokuwa wanasali ndani ya Msikiti huo.
Habari ID: 3473906 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/13
TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Wazayuni makatili na wauaji hawana uhusiano na dini yoyote ile.
Habari ID: 3473903 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/12
TEHRAN (IQNA)- Marjaa mkuu wa Kishia nchini Iraq kwa mara nyingine tena ametangaza uungaji mkono wake kwa 'mapambano ya kishujaa ya taifa lenye heshima la Palestina' katika kukabiliana na Wazayuni maghasibu na kutoa wito kwa mataifa yote huru duniani kuwaunga mkono Wapalestina.
Habari ID: 3473902 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/12
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, Wazayuni hawafahamu chochote zaidi ya lugha ya mabavu na akasisitiza kuwa, inapasa Wapalestina waongeze nguvu na muqawama wao ili kuwalazimisha watenda jinai hao wasalimu amri na kusimamisha hatua zao za kinyama.
Habari ID: 3473901 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/12
TEHRAN (IQNA)- Mabalozi wa kudumu wa nchini wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) katika Umoja wa Mataifa wametangaza azma yao ya kuhamisisha jamii ya kimataifa iunge mkono taifa la Palestina ambalo linakabiliwa na hujuma za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473899 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/11
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amemwandikia barua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kumjulisha matukio na mabadiliko yanayojiri katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3473894 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/10
TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Nigeria jana Ijumaa walijitokeza kwa wingi katika matembezi ya Siku ya Kimataifa ya Quds katika miji mikubwa ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Habari ID: 3473889 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/08