TEHRAN (IQNA) - Mashinikizo ya Marekani, Utawala wa Kizayuni wa Israel na Saudi Arabia ni chanzo kikuu cha serikali ya Nigeria kuendelea kumshikilia kinyume cha sheria kiongozi wa harakati ya Kiislamu nchini humo Sheikh Ibrahim Zakzaky.
Habari ID: 3472050 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/21
Taarifa ya IRGC
TEHRAN (IQNA) - Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC limetangaza kuwa limesimamisha meli moja ya mafuta ya Uingereza baada ya kukiuka sheria za kimataifa za ubaharia katika Lango Bahari la Hormuz.
Habari ID: 3472049 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/20
TEHRAN (IQNA) - Wahalifu wameuhujumu msikiti na kuvunjia heshima nakala za Qur'ani Tukufu maghairbi mwa Ujerumani.
Habari ID: 3472048 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/19
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekosoa vikali misimamo ya nchi za Ulaya na kushindwa kwao kutekeleza ahadi zao ndani ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kusisitiza kwa kusema: "Sisi ndio kwanza tumeanza kupunguza hadi zetu ndani ya mapatano hayo na bila ya shaka tutaendelea tu kupunguza utekelezaji wa ahadi zetu ndani ya JCPOA."
Habari ID: 3472047 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/18
TEHRAN (IQNA) - Wabunge katika Kongresi ya Marekani ambayo walidhalilishwa na Rais Donald Trump wa nchi hiyo wamesema hawatatishika.
Habari ID: 3472046 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/16
TEHRAN (IQNA) - Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Iran wameandamana kulalamikia kuendelea kushikiliwa kushikiliwa kinyume cha sheria Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.
Habari ID: 3472045 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/15
Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA) - Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza suala la kuimarika kwa nguvu na uwezo wa kujihami na kufanya mashambulizi wa wanamapambano katika kipindi cha miaka 13 iliyopita.
Habari ID: 3472042 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/14
TEHRAN (IQNA) -Watu 26 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia shambulio la kigaidi dhidi ya hoteli moja kusini mwa Somalia.
Habari ID: 3472041 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/13
TEHRAN (IQNA) - Watawala wa Saudi Arabia wamekasirishwa na kitendo cha Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) cha kuwaondosha nchini Yemen idadi kubwa ya wanajeshi wake.
Habari ID: 3472040 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/12
Balozi wa Palestina Tehran
TEHRAN (IQNA) - Balozi wa Palestina nchini Iran amesema utawala haramu wa Israel unapaswa kusitisha ukaliaji mabavu ardhi za Palestina huku akisisitiza kuwa, Palestina ni lazime irejee kwa Wapalestina.
Habari ID: 3472037 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/09
TEHRAN (IQNA) - Mwana wa Sheikh Ibrahim Zakzaky Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria ametahadharisha kupitia ujumbe aliotoa kwamba hali ya kimwili ya baba yake ni mbaya sana. Amesema karibu njia zote zimeshindikana kwa ajili ya kunusuru maisha yake.
Habari ID: 3472036 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/09
TEHRAN (IQNA) - Shirika moja la anga za mbali la nchini Russia ambalo hutayarisha chakula cha wanaanga (astronauts) kimesema kitaanza kutayarisha chakula halali maalumu kwa ajili ya Waislamu.
Habari ID: 3472033 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/07
TEHRAN (IQNA) - Vyuo vikuu vya umma nchini Indonesia vimetangaza kuwa vijana waliohifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu wanaweza kuingia katika vyuo vikuu pasina kufanya mtihani wa kawaida unaohitajika kuingia chuo kikuu.
Habari ID: 3472032 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/04
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema serikali ya Saudi Arabia ina wajibu na majukumu mazito ya kulinda usalama wa mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu na hadhi yao bila ya kueneza anga ya kipolisi.
Habari ID: 3472031 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/03
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa la Iran katu halitasalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani.
Habari ID: 3472030 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/02
TEHRAN (IQNA)- Maisan Yahya Muhammad, ni binti wa miaka sita ambaye kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambaye amehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.
Habari ID: 3472020 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/28
TEHRAN (IQNA)- Aghalabu ya Wapalestina wanapinga vikali mpango wa Muamala wa Karne na kikao cha uchumi kulichofanyika hivi karibuni mjini Manama, Bahrain.
Habari ID: 3472019 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/27
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa lengo kuu la pendekezo la Marekani la kufanya mazungumzo na Iran ni kutaka kulipokonya taifa la Iran silaha na sababu za nguvu na uwezo wake.
Habari ID: 3472018 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/26
Sheikh Issa Qassim
TEHRAN (IQNA) - Mwanazuoni maarufu wa Kiislamu nchini Bahrain, Ayatullah Sheikh Isa Qassim amelaani vikali hatua ya utawala wa Manama kuwa mwenyeji wa Kongamano la Kibiashara linalotazamiwa kuanza leo nchini humo kwa shabaha ya kuzindua mpango wa 'Muamala wa Karne'.
Habari ID: 3472017 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/25
TEHRAN (IQNA) – ‘Muamala wa Karne’ ambao umependekezwa na Marekani kwa lengo la kuunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel na kukandamiza ukombozi wa Palestina unaendelea kupingwa katika ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3472016 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/24