
Kikao hicho kilihudhuriwa na Hujjatul Islam Saeed Hardanian, mkuu wa makao ya Qur'ani katika ofisi ya mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu huko Khuzestan; Hadi Abyar, mkurugenzi wa maendeleo ya kiutamaduni na kisanii katika Eneo Huru la Arvand; pamoja na Mahmoud Hamidawi na wawakilishi wa taasisi za Qur'ani za mkoa huo. Kutoka upande wa Iraq walikuwepo pia Ali Radzi Shahed, mshauri wa mkuu wa Umoja wa Qur'ani wa Iraq, na Mustafa Zaki, mkuu wa ofisi ya Umoja wa Qur'ani wa Basra.
Katika kikao hicho, ilipitishwa azimio la kufanya sherehe ya kusaini makubaliano ya ushirikiano wa Qur'ani kati ya Khuzestan na Basra katika wiki chache zijazo. Pande zote mbili zilisistiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa Qur'ani unaojikita katika kujitengeneza kimaadili, kuimarisha mshikamano wa kijamii, na kuchangia ustaarabu wa Kiislamu.
Mambo makuu ya makubaliano yaliyodraftiwa ni pamoja na kufanya kozi za mafunzo ya pamoja kwa waqari na wahifadhi wa Qur'ani, kutekeleza programu za maelewano ya Qur'ani baina ya koo na makabila ya mikoa hiyo miwili, kuanzisha kituo cha kimataifa cha Qurani Tukufu baada ya kipindi cha miaka mitatu, na kuandaa matukio ya kimataifa ya Qur'ani katika Khuzestan, Eneo Huru la Arvand, na Basra. Aidha, imekubaliwa kuwa kozi za mafunzo ya pamoja zitaanza wiki ijayo.
Mipango mingine iliyowekwa ni pamoja na kufanya mkusanyiko wa kwanza wa Qur'ani wa pamoja katikati ya mwezi wa Shaaban kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria, kuunda vikundi maalumu vya kazi, kuwezesha mafunzo kwa wasomi 1,000 wa Qur'ani ndani ya kipindi cha miaka mitatu, kufanya kozi 100 za mafunzo, na kuanzisha vituo 40 vya undugu wa Qurani.
3495504