IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Hamburg,Ujerumani

20:49 - July 06, 2018
Habari ID: 3471585
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya 15 ya Qur'ani ya watoto na mabarobaro yamefanyika mjini Hamburg nchini Ujerumani wiki hii.

Baraza la Waislamu la Hamburg limeandaa mashindano hayo ya Qur'ani katika Msikiti wa Yildiz. Taarifa zinasema washiriki wa mashindano hayo walikuwa kutoka mataifa mbali mbali ni pia kutoka madhehebu mbali mbali za Kiislamu.

Aidha washiriki walishindana katika kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Mashindano hayo yalijumuisha makundi matatu ya watoto na mabarobaro walio kati ya umri wa miaak 10-13 na 14-17.

Kuna takribani Waislamu milioni nne nchini Ujerumani na hivyo kuufanya Uislamu kuwa dini ya pili kwa ukubwa nchini humo.

3727902

 

captcha