IQNA

Harakati ya Al Wifaq ya Bahrain yatangaza ‘Ijumaa ya Ghadhabu’ kulaani mapatano na Israel

20:49 - September 16, 2020
Habari ID: 3473175
TEHRAN (IQNA) – Harakati ya Al Wifaq ya Bahrain imetangaza ijumaa wiki hii kuwa ni ‘Ijumaa ya Ghadhabu’ kwa ajili ya kubainisha kuchikizwa na mpatano yaliyopfikiwa kati ya utawala haramu wa Israel na utawala wa Bahrain.

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mwafaka wa Kiislamu na Kitaifa nchini Bahrain (Al Wifaq) amesema kuwa, kutiwa saini hati ya mapatano baina ya Bahrain, Umoja wa Fame za Kiarabu (UAE) na utawala wa Kizayuni wa Israel ni ni jinai ya kihistoria.

Sheikh Hussein al-Daihi, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mwafaka wa Kiislamu na Kitaifa nchini Bahrain (Al Wifaq) amebainisha kuwa, tawala za Bahrain na UAE zimechukua hatua ya kuanzisha uhusiano na utawala ghasibu wa Israel na hivyo kutenda jinai kubwa kwa hatua yao hiyo kwani zimefanya juhudi za kuuhalalisha utawala huo unaotenda jinai kila leo dhidi ya Wapalestina.

Sheikh Hussein al-Daihi, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mwafaka wa Kiislamu na Kitaifa nchini Bahrain (Al-Wifaq) amebainisha kuwa, tawala za Bahrain na Imarati zimechukua hatua ya kuanzisha uhusiano na utawala ghasibu wa Israel na hivyo kutenda jinai kubwa kwa hatua yao hiyo kwani zimefanya juhudi za kuuhalalisha utawala huo unaotenda jinai kila leo dhidi ya Wapalestina.

Taarifa ya Twitter ya Al Wifaq imesema Wabahrain watashriki katika maandamano yaliyopewa jina la 'Ijumaa ya Ghadhabu Kuhusu Quds'

Kadhalika, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mwafaka wa Kiislamu na Kitaifa nchini Bahrain (Al-Wifaq) amesisitiza kuwa, daima wananchi wa Bahrain watakuwa pamoja na Wapalestina katika harakati zao za mapambano za kupigania ukombozi wa ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.

Katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja tangu Imarati ilipotangaza kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel, utawala wa kiimla na kidikteta wa Bahrain nao umefuata mkumbo huo, ambapo tarehe 11 Septemba, rais wa Marekani alitangaza rasmi kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Bahrain na utawala wa Kizayuni unaoikalia kwa mabavu Palestina. Usaliti huo wa nchi hizo za Kiarabu umelalamikiwa na unaendelea kulalamikiwa vikali.

3923463

Kishikizo: bahrain ، UAE ، quds ، palestina ، israel
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :