IQNA

Maulidi

‘Sherehe za Maulid Mashhad, Iran zinajumuisha vikao vya kusoma Qur'ani Tukufu

15:40 - September 17, 2024
Habari ID: 3479447
IQNA – Wasimamizi wa Haram ya Imam Ridha (AS) katika mji wa Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran wamepanga vikao kadhaa vya Qur'ani Tukufu, wakibainisha kuwa zinalenga kulinda urithi wa Mtume Muhammad (SAW).

Hujjatul Islam Seyyed Masoud Mirian, Mkurugenzi wa Kituo cha Masuala ya Qur'ani katika Haram Tukufu ya Imam Ridha (AS) amesema kuwa, vikao 12 vya Qur'ani vimepangwa katika eneo lote la kaskazini mashariki mwa Iran la Khorasan Razavi wakati Wiki ya Umoja wa Kiislamu ikiadhimishwa kote Iran.

"Wiki ya Umoja ni fursa muhimu ya kuimarisha udugu na umoja miongoni mwa Waislamu," aliwaambia waandishi habari Jumatatu.

"Mtukufu Mtume (SAW) aliacha mirathi mbili za thamani: Qur'ani Tukufu na Ahlul-Bayt (AS) kama amana kwa umma wa Kiislamu," alisema na kuongeza, "Kwa kuzifuata, tunaweza kuhifadhi umoja na kuzuia migawanyiko. .”

Amebainisha kuwa mikusanyiko 12 ya Qur'ani itafanyika kuanzia Septemba 16 hadi 19 katika misikiti ya miji na vijiji vya Torbat-e Jam, Salehabad, Khaf, Taybad na Bakharz.

Maqari na  wahifadhi wa Qur'ani wa kimataifa, kitaifa na kieneo watakuwa wenyeji wa mijumuiko hiyo ya umma wakati wa Maulidi.

"Mikusanyiko hii inafanyika kwa lengo la kukuza mafundisho ya Qur'ani, kulinda turathi zenye thamani za Mtukufu Mtume Muhammad (SAW), na kusisitiza umoja kwa kuwepo wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani wa kitaifa na kieneo," alisisitiza.

Ikumbukwe kuwa miaka 1499  tarehe 12 Mfunguo Sita Rabiul Awwal miaka 53 kabla ya Hijria, kwa kauli ya baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu akiwemo Mas'udi, alizaliwa Mtume Muhammad (SAW).

Wanachuoni wengine wa Kiislamu wanaamini kwamba, Mtume Muhammad (saw) alizaliwa tarehe 17 Rabiul Awwal mwaka huohuo. Kwa msingi huo, Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu Amrehemu), muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitangaza kipindi cha kuanzia tarehe 12 hadi 17 Rabiul Awwal kila mwaka kuwa ni Wiki ya Umoja kati ya Waislamu kote duniani.

Wiki ya umoja ni fursa nzuri ya kuzikurubisha nyoyo za Waislamu na kuimarisha umoja na mshikamano wao katika kukabiliana na maadui wa ulimwengu wa Kiislamu.  

 3489934

Habari zinazohusiana
captcha