IQNA

Mwanazuoni wa Ahul Sunna nchini Iran

Umoja unaweza kutatua matatizo ya Ulimwengu wa Kiislamu

18:20 - June 24, 2022
Habari ID: 3475419
TEHRAN (IQNA) – Mwanazuoni mwandamizi wa Kisunni nchini Iran na mjumbe wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu amesema matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu yanaweza kutatuliwa kwa umoja.

Akizungumza na  Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), Mawlawi Is'haq Madani amesisitiza haja ya kuimarisha umoja katika ulimwengu wa Kiislamu. Nukuu kutoka kwa maneno yake ni kama ifuatavyo:

Hivi karibuni Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu alizungumzia kuhusu umoja kati ya Waislamu wa Shia na Sunni. Hii, bila shaka, si mara ya kwanza kwani mara kwa mara ametaja suala hili na analipa umuhimu mkubwa suala la umoja wa Waislamu. Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu ni dhihirisho la hii. Imam Khomeini –Mwenyezi Mungu Amrehemu- Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia alitilia mkazo juu ya umoja.

Mwenyezi Mungu SWT anasema katika Aya ya 103 ya Surah Al Imran: “Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka.”

Kwa hivyo kutokana na msisitizo wa Qur’ani, tunahitaji kuwaalika watu kwenye umoja na kuuimarisha mashikamano huo.

Wakati wengine baadhi  wanafikiri kufikia umoja ni jambo gumu, inawezekana na si jambo gumu kama kuna mapenzi miongoni mwa Waislamu. Wanazuoni wakubwa wa Shia na Sunni huko nyuma walikuwa na umoja huku wakiwa na mitazamo tofauti katika baadhi ya masuala. Tofauti hizo za mawazo na fikra ni muhimu kwa maisha na hakuna mtu anayeweza kufikiri tunaweza kuishi bila kuwa na tofauti yoyote ya mawazo. Hata hivyo, licha ya kuwa na tofauti, watu wanaweza kufikia umoja kulingana na maoni yanayofanana.

Umoja wa Waislamu ni suala muhimu sana na linaweza kutatua matatizo yanayoukabili ulimwengu wa Kiislamu.

4065258 

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :