IQNA

Afisa wa Hizbullah: Kadhia ya Ukraine inaonyesha kosa la kuitegemea Marekani

14:02 - February 26, 2022
Habari ID: 3474977
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Baraza Kuu la harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema ni makosa kwa baadhi ya nchi kutegemea uungwaji mkono na himaya ya Marekani, na kwamba kadhia ya Ukraine imethibitisha tena ukweli huo.

Akizungumzia vita vya Ukraine, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Hizbullah, Sayyid Hashem Safieddine amesema kuwa Lebanon itajiondoa katika majanga yote kwa ukombozi wa kweli na kujiondoa kwenye udhibiti wa utawala wa Marekani.

Ameongeza kuwa Marekani na nchi za Magharibi ziliwachochea Waukraini na kuwaahidi msaada na ushirikiano, lakini walipogundua kuwa maslahi yao yalikuwa hatarini, wamekengeuka ahadi zao na kulinda maslahi yao.

Mwenyekiti wa Baraza Kuu ya Hizbullah ya Lebanon ameeleza kuwa Rais wa Marekani, Joe Biden baada ya kuliona suala hilo kuwa zito ametangaza kuwa nchi yake haitashiriki katika vita vya Ukraine. Ameongeza kuwa: "Hivi ndivyo Marekani inavyowatumbukiza watu kwenye moto wa fitina nchini Lebanon kisha inawaacha mkono.” 

Huku hayo yakijiri, mapigano yakiendelea katika viiunga vya mji mkuu wa Ukraine, Kiev baada ya kusita kwa muda mfupi usiku wa kuamkia leo, Rais wa Ukraine amekata pendekezo la Marekani lya kumsaidia kutoroka nchini humo.

Rais Volodymyr Zelenskyy amewaambia Wamarekani kwamba: Vita iko nchini Ukraine. Tunahitaji silaha na si kutoroka nchi."

Hayo yamefichuliwa na afisa mmoja wa ngazi za juu wa shirika la ujasusi la Marekani.

Mapigano ya mitaani yameibua baina ya wanajeshi wa Ukraine na vikosi vya Russia katika mji mkuu wa Kyiv, ambao ulikumbwa na mashambulio na milipuko usiku kucha.

Vikosi vya jeshi la Russia vinaripotiwa kuwa kwenye viunga vya mji mkuu wa Ukraine katika kile kinachoonekana kama harakati za kuuzingira, baada ya mashambulizi ya anga kwenye miji na kambi za kijeshi kote nchini nchini humo.

Mashambulizi hayo yalianza Alkhamisi iliyopita baada ya Rais Vladimir Putin wa Russia kutangaza kwamba jeshi la nchi hiyo limeanzisha "operesheni maalumu ya kijeshi" katika eneo la Donbass nchini Ukraine na kwamba lengo la operesheni hiyo ni kuiondoa Ukraine katika hali ya kijeshi na kwamba hana nia ya kuvamia ardhi ya nchi hiyo.  

4038829

Kishikizo: ukraine hizbullah russia
captcha