Sayyid Hassan Nasrallah alisema hayo jana Ijumaa katika hotuba yake aliyoitoa kwa mnsaba wa Maadhimisho ya Siku ya Maskauti wa Al-Mahdi na kueleza kuwa, vyombo vya habari vya Waarabu vimeeneza uvumi huo kwa kunukuu duru za kijeshi za Ukraine.
Sayyid Nasrallah amenukuliwa na televisheni ya al-Manar akisisitiza kuwa, "Nakadhibisha vikali uvumi wa namna hii. Huu ni urongo na uvumi usio na msingi wowote. Hizbullah haijatuma wapiganaji au wataalamu wowote Ukraine."
Hivi karibuni pia, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon alisisitiza kuwa, mgogoro wa Ukraine umedhihirisha wazi undumakuwili na mmomonyoko wa kimaadili wa Wamagharibi.
Kwengineko katika hotuba yake ya jana Ijumaa, Sayyid Hassan Nasrallah ametoa mwito kwa serikali ya Lebanon kuunda kamati ya dharura ya kuchunguza athari za kiuchumi kutokana na mgogoro wa Ukraine, hususan suala la bei za bidhaa muhimu.
4044043