IQNA

Jinai za kivita za Israel
18:50 - May 25, 2022
Habari ID: 3475294
TEHRAN (IQNA)- Mashirika kadhaa ya kutetea haki za Wapalestina yameikabidhi Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) maelezo ya kina kuhusu jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu zilizofanywa na utawala wa Israel wakati wa hujuma zake za kijeshi dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza mwaka 2021.

Mashirika ya haki za binadamu ya Palestina, ikiwa ni pamoja na al-Haq, al-Mezan, na Kituo cha Haki za Binadamu cha Palestina (PCHR), ambayo hufuatilia na kuandika ripoti kuhusu ukiukaji wa haki unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel yaliwasilisha ripoti kwa mahakama hiyo yenye makao yake makuu The Hague ili kuharakisha uchunguzi kuhusu uhalifu na ukiukaji unaofanywa na utawala wa Tel Aviv na kuwafikisha wahusika kwenye vyombo vya sheria.

"Shambulio la Mei 2021 huko Gaza ni mfano wa hivi karibuni zaidi wa mfululizo wa mashambulizi ya kijeshi yenye uharibifu mkubwa na yenye lengo la kusababisha uharibifu usio na uwiano na mateso kwa raia wa Ukanda wa Gaza, eneo ambalo linakabiliwa na mzingiro unaotekelezwa na Israel kinyume cha sheria kwa mudawa miaka 15, ” alisema Raji Sourani, Mkurugenzi wa PCHR.

Tel Aviv ilianzisha kampeni ya kikatili ya kuushambulia Ukanda wa Gaza mnamo Mei 10, 2021, kufuatia hatua za kulipiza kisasi za Wapalestina kufuatia uvamizi wa kikatili uliotekelezwa na utawala wa Israel dhidi ya waumini wa Msikiti wa al-Aqsa na mipango ya utawala huo kuzilazimisha familia kadhaa za Kipalestina kuhama nyumba zao za jadi huko Sheikh Jarrah, kitongoji cha Quds (Jerusalem) Mashariki inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo dhalimu.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza, Wapalestina 260 waliuawa shahidi katika mashambulizi ya Israel, ikiwa ni pamoja na watoto 66 na wanawake 40. Takriban Wapalestina  wengine 1,948 pia walijeruhiwa.

Katika kukabiliana hujuma za Israel, harakati za mapambano ya Kiislamu au muawama huko Palestina, zikiongozwa na Hamas, ziianzisha Operesheni ya Upanga wa al-Quds Upanga na kuvurumisha zaidi ya makombora zaidi ya 4,000 katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu  na kuua Waisrael wasiopungua 12.

Israel ilishtushwa na msururu wa maroketi na makombora kutoka Gaza, na hivyo ikalazimika kutangaza usitishaji vita wa upande mmoja Mei 21, ambao makundi ya Palestina yalikubali kusitisha mapigano kwa upatanishi wa Misri.

Kwingineko katika ripoti zao, makundi ya haki za binadamu ya Palestina yamesema uhalifu uliofanywa na Israel  dhidi ya raia wa Palestina na miundo msingi ya kiraia Gaza ni uhalifu wa aina yake ambayo haujafanywa maeneoe mengine ya dunia.

Rights Groups Urge ICC to Probe Israeli War Crimes in Last Year’s Gaza War

Mwendesha mashtaka mkuu wa zamani wa ICC, Fatou Bensouda mwaka jana alitangaza kuanzishwa kwa uchunguzi wa uhalifu wa kivita katika maeneo ya Palestina, ambayo yamekuwa yakikaliwa kwa mabavu na  Israel tangu mwaka 1967.

Alisema uchunguzi wake utafanywa "kwa uhuru, bila upendeleo na bila upendeleo, bila woga au upendeleo." Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA) ilikakaribisha tangazo hilo.

Ni "hatua iliyosubiriwa kwa muda mrefu ambayo inaenda sambamba na harakati zisizo na kikomo za Palestina za kufuatilia haki na uwajibikaji, ambazo ni nguzo muhimu za amani ambayo watu wa Palestina wanatafuta na wanastahili", wizara ya mambo ya nje ya PA ilisema katika taarifa wakati huo.

3479047

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: