IQNA

Wabunge wa Kuwait wataka wanachama wa BJP India wapigwe marufuku

19:31 - February 21, 2022
Habari ID: 3474955
TEHRAN (IQNA)- Wabunge kadhaa nchini Kuwait wametaka wanachama wa chama tawala India, Bharatiya Janata (BJP) wapigwe marufuku kuingia nchini humo kutokana na kuhusika kwao na ukandamizaji wa Waislamu nchini India.

Pendekezo hilo limekija kufuatia kupigwa marufuku wanafunzi wa kike Waislamu kuvaa Hijabu katika taasisi za kielimu jimboni Karnataka.

Mwanaharakati na mtatezi wa haki Majbal Al Sharika amesambaza barua ya wabunge hao katika ukurasa wake wa Twitter huku akisema India inapaswa kufahamu sera zake za ndani ya nchi zina matokeo mabaya kimataifa.

Amesema ni wakati sasa Waislamu duniani kuungana kuwatetea wanawake Waislamu India ambao wanadhalilishwa hadharani kutokana na kuvaa Hijabu.

Kushadidi kwa mizozo na hitilafu juu ya vazi la hijabu la wasichana na wanawake wa Kiislamu katika vyuo na taasisi za elimu katika jimbo la Karnataka huko kusini mwa India kumezusha hali ya wasiwasi na hofu kwa jamii za Waislamu nchini humo.

3477900/

Habari zinazohusiana
captcha