IQNA

Harakati za Muqawama

Ujumbe wa Hamas ya Palestina wakutana na Kiongozi wa Hizbullah ya Lebanon

17:14 - August 28, 2022
Habari ID: 3475695
TEHRAN (IQNA)- Ujumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS umeonana na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon mjini Beirut, ukiwa ni ushahidi wa kuzidi kushikamana kambi ya muqawama katika eneo hili.

Kwa mujibu wa taarifa, ujumbe huo wa ngazi za juu wa HAMAS ambao umeonana na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrallah, unaongozwa na Kamanda Saleh al-Arouri, mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa harakati ya HAMAS.

Hadi tunapokea habari hii hakukuwa kumetolewa taarifa za kina kuhusu malengo ya ujumbe huo mzito wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS kwenda kuonana na Sayyid Hassan Nasrallah. 

Jana pia, ujumbe huo wa ngazi za juu wa HAMAS ulikutana na Ziyad al-Nakhalah, Katibu Mkuu wa Jihad al Islami ya Palestina.

Katika mazungumzo hayo ya jana, pande hizo mbili zilijadiliana matukio ya hivi karibuni ya Palestina na ya eneo hili kiujumla, njama za utawala wa Kizayuni za kutoa pigo kwa kambi ya muqawama katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu na matokea ya vita vya hivi karibu vya siku tatu vilivyoanzishwa na Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza pamoja na ushujaa na kujitolea muhanga mateka wa Kipalestina kwenye jela za kuogofya za Wazayuni.

Jeshi la Kizayuni lilifanya jinai kubwa katika vita hivyo vya kivamizi vya siku tatu. Liliua shahidi Wapalestina 49 na kujeruhi zaidi ya 360 wengine. Makundi ya mapambano ya Palestina yalijibu jinai hiyo kwa kuitwanga kwa mamia ya makombora miji na vitongoji vya walowezi wa Kizayuni ukiwemo Tel Aviv, mji mkuu wa utawala wa Kizayuni. 

4081355

captcha