IQNA

Muqawama

Kiongozi wa Hizbullah: Makamanda wa Muqawama hawajifichi, Wazayuni watalia

11:40 - August 02, 2024
Habari ID: 3479210
IQNA-Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, katika kambi ya muqawama, wakuu na makamanda wa kambi hiyo hawajifichi bali wako katikati ya medani ya mapambano na wanakufa shahidi kwenye medani hiyo.

Sayyid Hassan Nasrallah alisema hayo jana kwenye hotuba aliyoitoa katika shughuli ya maziko ya shahid Fuad Ali Shukr, mmoja wa makamanda wa ngazi za juu wa Hizbullah ya Lebanon. Shughuli hiyo imefanyika katika Husainia ya Mashahidi huko kusini mwa Beirut, mji mkuu wa Lebanon shughuli ambayo imeambatana pia na kumbukumbu ya kuuawa shahidi Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS. Sayyid Nasrallah ametumia fursa hiyo kutoa pongezi na mkono wa pole kwa Brigedi za Izuddin Qassam, Tawi la Kijeshi la HAMAS na kwa taifa zima la Palestina.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, sisi tuko pamoja na HAMAS kweenye muqawama na mapambano ya kufa shahidi katika njia ya haki na tuna yakini kwamba ushindi ni wetu.

Amesema kuwa, adui Mzayuni ameshambulia jengo lililojaa raia wakati walipoendesha shambulio la kigaidi la kumuua shahidi Kamanda Fuad Shukr ambapo miongoni mwa watu waliouawa shahidi katika jinai hiyo alikuwemo pia mshauri mmoja wa kijeshi wa Iran na makumi ya watu wamejeruhiwa.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza pia kuwa, shambulio lililofanywa na Wazayuni huko kusini mwa Lebanon halikuwa la kigaidi tu, bali lilikuwa ni shambulio dhidi ya jengo la ghorofa ambalo ni makazi ya raia.

Ameongeza kuwa, siku chache kabla ya kufanya shambulio hilo, adui Mzayuni alidai kuwa, atafanya shambulizi la kulipiza kisasi lakini sisi hatukubaliani kabisa na madai hayo ya uongo ya adui.

Amesema, shambulio katika eneo la kusini mwa Beirut lilikuwa ni muendelezo wa vita vya Israel na Marekani katika eneo la Asia Magharibi akisisitiza kuwa, tunakanusha madai yote yaliyotolewa na Marekani na utawala wa Kizayuni na kwamba adui Mzayuni asubiri majibu makali mno kutoka kwa kambi ya muqawama.

3489339

Habari zinazohusiana
captcha