IQNA

Msomaji Qur'ani wa Misri

Msomaji Qur’ani Misri anayeiga sauti Abdul Basit (+Video)

21:32 - September 05, 2022
Habari ID: 3475737
TEHRAN (IQNA) – Sheikh Mohammed Buhairi Abdul Fattah ni qarii wa Kimisri ambaye usomaji wake wa Qur’ani Tukufu unawakumbusha wasikilizaji enzi nzuri ya usomaji wa Qur’ani nchini humo za Sheikh Abdul Basit Abdul Samad.

Hivi karibuni Sheikh Buhairi alizungumza na televisheni ya Al-Mihwar, akisema alianza kusoma Qur'ani Tukufu akiwa na umri wa miaka 15.

Alianza usomaji wake wakati ambapo maqari wakubwa kama Abdul Basit Abdul Samad, Abolainain Shoaisha, Mohammed Ali al-Banna, Mustafa Ismail na Mohammed Sidiq Minshawi walikuwa wasomaji wakuu wa Qur'ani nchini.

"Nilijifunza mengi kutoka kwao," alisema katika mahojiano hayo.

Buhairi aliongeza kuwa tangu mwanzo amezingatia sana kujifunza na kuzingatia sheria za Tajweed katika usomaji wake.

Amesisitiza kuwa, kigezo muhimu zaidi cha usomaji mzuri na sahihi wa Qur'ani ni kuzingatia sheria za Tajweed.

Tajweed ni seti ya sheria za matamshi sahihi ya herufi na sifa zao zote na kutumia njia mbali mbali za usomaji Qur’ani Tukufu.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100. Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.

Shughuli za Qur'ani ni za kawaida sana katika nchi ya kasakini mwa Afrika ambapo ina idadi kubwa ya wasomaji Qur’ani bora zaidi duniani.

3480216

Kishikizo: msomaji qurani ، abdul basit ،
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha