IQNA

Uislamu Marekani

Chuo Kikuu cha Arizona Marekani kuelimisha wasio Waislamu kuhusu Uislamu

21:22 - September 25, 2022
Habari ID: 3475840
TEHRAN (IQNA) – Chuo Kikuu cha Jimbo la Arizona (ASU) kilifungua Kituo cha Uzoefu wa Kiislamu nchini Marekani muhula huu.

Kituo hicho kinalenga kuhudumia idadi ya wanafunzi Waislamu na kuwaelimisha wengine kuhusu Uislamu.

Ingawa kituo hicho hakina makao maalumu lakini kinasema lengo lake kuu ni kubadilisha taswira kuhusu  Waislamu na Uislamu nchini Marekani kwa kushirikiana na jumuiya za Kiislamu za eneo hilo, kufanya utafiti juu ya jumuiya na kuandaa matukio ya uhamasishaji.

"Uislamu na Waislamu daima wamefafanuliwa, hasa tangu 9/11, ima kama tishio la usalama au kama watu wa nje," alisema profesa msaidizi wa masomo ya kidini, Chad Haines.

Haines na mkurugenzi mwenza na profesa wa historia Yasmin Saikia wanatumia kituo hicho kupambana na taswira hii na kufundisha kuhusu misimamo sahihi ya Waislamu nchini Marekani.

Haines alisema kihistoria sauti za Waislamu zimekuwa zikizimwa, na mara tu wanaporuhusiwa kuzungumza, maneno yao "hupangwa" na kile ambacho wengine wanataka kusikia.

Saikia alisema kuna historia kubwa kuhusu utambulisho wa Kiislamu ambayo "haipo katika masimulizi ya historia" kwani mara nyingi husahaulika kuwa Marekani ilijengwa na watumwa wengi wa Kiislamu. Kituo kilichoanzishwa kinalenga kuangazia historia hii ili kuweka vyema nafasi ya raia wa Kiislamu nchini Marekani.

Muhula uliopita, Msahafu ulipatikana ukiwa imeharibiwa katika Chumba cha Tafakari ya Dini Mbalimbali katika Maktaba ya Hayden kwenye kampasi ya ASU ya Tempe. Haines alisema sehemu ya malengo kituo walichoanzisha ni kuzuia na matukio kama haya kwa kutoa ujuzi juu ya jamii ya Kiislamu.

3480608

Kishikizo: uislamu ، marekani ، waislamu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha