
Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Muslims Around The World, maonesho hayo ni miongoni mwa matukio mashuhuri ya Ramadhani nchini humo. Yanatoa jukwaa jumuishi linalokutanisha vipengele vya kidini, kiuchumi na kijamii, kwa kuwapa waonyeshaji na wajasiriamali fursa ya kuwasilisha bidhaa na huduma zao , hususan katika sekta ya bidhaa 'Halal' na shughuli mahsusi za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Waandalizi walilenga kuvutia maelfu ya wageni, jambo litakalowawezesha washiriki kuimarisha uwepo wao wa kibiashara na kuwasiliana moja kwa moja na hadhira pana yenye dhamira na mshikamano wa kijamii.
Sambamba na maonesho ya kibiashara, tukio hilo litapambwa na mihadhara ya kidini, semina na warsha za kielimu, shughuli za kitamaduni, swala za jamaa pamoja na maandalizi ya futari za pamoja. Huduma mbalimbali za kijamii na ushauri nasaha pia zitatolewa kwa jamii.
Kupitia programu na shughuli zake zilizoandaliwa kwa upeo mpana, tukio hili linalenga kuiandaa jamii ya Kiislamu kuupokea mwezi wa Ramadhani katika mazingira yanayochanganya ibada, elimu na mshikamano wa kijamii , katika roho ya taqwa na udugu.
Waandalizi wametoa mwaliko wa wazi kwa taasisi na wajasiriamali kushiriki, iwe kwa kuonesha bidhaa zao au kwa kujiunga kama wadau na wadhamini. Wamesisitiza kuwa maonesho hayo ni fursa adhimu ya kuimarisha uwajibikaji wa kijamii, kuuchochea uchumi wa ndani, na kuendeleza tunu za mshikamano wakati wa Ramadhani , hatua itakayochangia athari endelevu za kidini, kijamii na kiuchumi kwa Waislamu wa Benin.
Maonesho ya “FIRam 2026” yanaakisi mwelekeo unaokua wa kuandaa matukio yanayounganisha utambulisho wa Kiislamu na maendeleo ya kijamii, yakithibitisha nafasi ya Ramadhani kama kituo cha kina cha imani, matendo na mshikamano.
Benin ni taifa linalozungumza Kifaransa lililoko Afrika Magharibi. Kwa mujibu wa makadirio ya hivi karibuni ya mwaka 2020, asilimia 52.2 ya wakazi wake ni Wakristo, asilimia 24.6 ni Waislamu, asilimia 17.9 wanafuata dini za jadi za Kiafrika, na asilimia 5.3 wanafuata imani nyinginezo.
3496399