IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Mkutano wa Qur'ani mjini Baghdad wahimiza kulinda matukufu ya kidini

18:34 - July 28, 2023
Habari ID: 3477350
BAGHDAD (IQNA) - Washiriki katika mkutano wa kutetea Qur'ani Tukufu nchini Iraq wamesisitiza haja ya kutunga sheria za kimataifa zinazoharamisha kuvunjiwa heshima matakatifu ya kidini.

Mkutano huo ulifanyika siku ya Jumatano na Idara ya Kitaifa ya Sayansi ya Qur'ani yenye mafungamano na Idara ya Waqfu ya Shia ya Iraq.

Katika taarifa ya mwisho, washiriki  hao pia wamezitaka taasisi na vituo vya Qur'ani na waumini wote wa Qur'ani Tukufu duniani kulaani vitendo vya hivi karibuni vya kuvunjiwa heshima Qur'ani nchini Uswidi na Denmark.

Ifuatayo taarifa ya mwisho ya mkutano huo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

"  Lau kuwa tumeiteremsha hii Qur'ani juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeli uona ukinyenyekea, ukipasuka kwa khofu ya Mwenyezi Mungu. Na hiyo mifano tunawapigia watu ili wafikiri." (Aya ya 21 ya Surah Al-Hashr)

 

Muaminini Mwenyezi Mungu Mtukufu

Mwenyezi Mungu amemuumba mwanaadamu kuwa mtukufu maadamu atashikamana na utiifu wake na akatembea kwa njia yake sahihi aliposema (anayetaka utukufu, utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu). Msingi muhimu zaidi wa utukufu ni kushikamana na Kitabu Kitakatifu cha Mwenyezi Mungu na kukitakasa na kukilinda dhidi ya kuvunjiwa heshima na kudhalilishwa.

Tumesimama hapa kulaani kitendo vya  aibu na kiovu cha kuchoma moto Qur’ani Tukufu ambacho  Waislamu wameshuhudia namna kilivyoidhinishwa na serikali ya Uswidi na Denmark. Kitendo hiki cha aibu kimerudiwa mara nyingi, kwa hivyo ni lazima tuchukue msimamo thabiti wa kuunga mkono na kutetea Qur’an Tukufu: “Ikiwa mtasaidia  katika Njia ya Mwenyezi Mungu, Yeye atakunusuruni.”

Kongamano la waalimu na wasomaji wa Qur'ani Tukufu kimeamua  yafuatayo:

1- Kuwasilisha shukurani kubwa na shukurani kwa marjaa na viongozi wakuu wa Kiislamu hasa Ayatullah Seyed Ali al-Sistani- Mwenyezi Mungu Mtukufu amlinde- kwa kuandikia barua Umoja wa Mataifa na kulaani hatua za kuvunjia heshima matukufu ya kidini.

2- Kuunga mkono hatua za serikali ya Iraq katika kufunga ubalozi wa Uswidi mjini Baghdad na kumuondoa balozi wa Iraq nchini Uswidi.

3- Kuzitaka taasisi na vituo vya Qur'ani Tukufu na waumini wote wa Qur'ani Tukufu duniani kulaani kukemea vitendo hivyo na pia kuzishinikiza serikali zao kuchukua hatua za kuzuia vitendo hivyo.

4- Kuzitaka mahakama za Kimataifa kutunga sheria ya kimataifa inayowatia hatiani wale wanaokiuka vitabu vitukufu hasa kwa Qur'ani Tukufu.

5- Kutoa wito kwa jumuiya zote za Waislamu nchini Uswidi kuwezesha shughuli za Qur'ani na kuandaa vikao vya Qur'ani na vikao katika viwanja vya umma baada ya kupata ruhusa kutoka kwa serikali ya Uswidi.

6- Kuzitolea wito kwa taasisi za Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni na taasisi zinazo simamia Haram Takatifu kuunga mkono harakati za Qur'ani Uswidi na Denmark na pia katika nchi nyingine za Magharibi hasa kufungua matawi  ya vituo vya Qur'ani Tukufu  katika nchi hizi ili kuandaa  kozi za Qur'ani ili kuhudumia jamii za Kiislamu kwa ujumla.

 
 
4158492
Habari zinazohusiana
captcha