IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Mashambulio Israel dhidi ya Gaza yanachochea chuki dhidi ya Uislamu Ulimwenguni

21:06 - January 09, 2024
Habari ID: 3478172
IQNA – Vita vya utawala haramu wa Israeli dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza vimezidisha hisia dhidi ya Uislamu duniani (Islamophobia) kote, anasema mwanachama wa kundi kubwa zaidi la kutetea haki za Waislamu nchini Marekani.

Corey Saylor, mkurugenzi wa utafiti na utetezi katika Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani, au CAIR, aliliambia Shirika la Anadolu, kwamba sababu kuu ya chuki dhidi ya Uislamu ni "mauaji ya halaiki yanayoendelea Gaza," ambapo mashambulizi ya anga ya Israel yameua zaidi ya Wapalestina 23,000. wengi wao wakiwa raia hasa wanawake na watoto, tangu Oktoba 7.

Alisema kuwa nchini Marekani, Waislamu na washirika wao wanakabiliwa na wimbi la chuki kwa kuunga mkono "haki ya Wapalestina ya kuishi, kutokoloniwa na kutoishi chini ya ubaguzi wa rangi."

Aidha alibainisha kuwa chuki dhidi ya Uislamu "imekita mizizi zaidi katika jamii ya Magharibi, kwa ujumla," na kwamba "iko nje ya udhibiti" duniani kote.

Alisema dunia inakumbwa na wimbi baya zaidi la chuki dhidi ya Uislamu tangu Desemba 2015, wakati Donald J. Trump, aliyekuwa mgombea urais wa chama cha Republican wakati huo alipotoa wito wa kupigwa marufuku kabisa Waislamu kuingia nchini humo.

CAIR ilipokea ripoti 2,171 au malalamiko ya ubaguzi wa Waislamu katika siku 57 za kwanza baada ya utawala wa Israel kuanza vita vyake dhidi ya Gaza, Saylor alisema. Idadi hiyo iliwakilisha karibu nusu ya jumla ya kesi ambazo kundi lilikuwa nazo mnamo 2022.

Ametoa mifano kadhaa ya ukatili na unyanyasaji dhidi ya Waislamu nchini Marekani, ikiwa ni pamoja na:

- Kuchomwa kisu na kuuawa mvulana wa miaka 6 Mpalestina na Marekani, Wadea al-Fayoume wakati akiwa na mamake, Hanaan Shahin, nyumbani kwao huko Illinois. Walishambuliwa  mwenye nyumba waliokuwa wamekodisha ambaye alipiga kelele dhidi ya Uislamu na kuonyesha kukasirishwa na hali huko Israel.  Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama mvulana huyo alidungwa kisu mara 26 huku mama yake kujeruhiwa vibaya katika hujuma hiyo. Mwenye nyumba, Joseph M. Czuba, 71, alishtakiwa kwa mauaji na uhalifu wa chuki.

- Matumizi ya magari kama silaha dhidi ya waandamanaji katika maeneo mengi, na kufyatua risasi  hewani au hata kuwafyatulia risasi wanaounga mkono "ubinadamu wa Palestina," Saylor alisema.

- Kulenga wanafunzi wanaounga mkono Palestina katika  vyuo vikubwa kama vile  Chuo Kikuu cha Harvard.

- Kuripotiwa kwa wafanyikazi waliohudhuria maandamano dhidi ya Israel. "Imekuwa ngumu sana miezi michache iliyopita kwa Waislamu nchini Marekani," Saylor alisema.

Pia alilaumu vyombo vya habari kwa kueneza habari potofu na dhana potofu kuhusu Waislamu, kama vile ripoti za uwongo za watoto kukatwa vichwa na Hamas mnamo Oktoba 7.

Alisema kuwa vyombo vingi vya habari vimeruhusu simulizi za chuki dhidi ya Uislamu kushamiri kwenye majukwaa yao, na kwamba taarifa kuhusu Waislamu "kwa ujumla ni mbaya sana" na watu wanaosema mambo ya kutisha kuhusu Uislamu na Waislamu hupewa nafasi ya kuzungumza katika vyombovya habari.

Alisema kuwa Israel imetumia dhana potofu dhidi ya Waarabu na Uislamu kusukuma ajenda yake kwa miongo kadhaa, na kwamba serikali ya Marekani pia inaendeleza simulizi hizo.

/3486743

Habari zinazohusiana
captcha