IQNA

Diplomasia

Rais Raisi asema bara Afrika lina nafasi muhimu katika sera ya kigeni za Iran

9:38 - March 02, 2024
Habari ID: 3478439
IQNA-Rais Seyed Ebrahim Raisi wa Iran amesisitiza kuwa, bara la Afrika lina nafasi muhimu katika sera za kigeni za serikali ya Iran na kuongeza kuwa: "Uhusiano na Afrika kwa ujumla na hasa nchi za Kiislamu barani Afrika una nafasi maalum sana katika sera zetu za kigeni."

Kabla ya kuondoka Tehran kuelekea Algeria mapema Jumamosi, Rais wa Iran amesema kwamba kwanza tunapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kushiriki kwa wingi wananchi kwenye vituo vya kupigia kura na akasema: "Lazima niwashukuru wananchi kwa uwajibikaji wao."

Kuhusu safari yake ya Algeria amesema kuwa safari hii ni kwa mwaliko wa Rais wa Algeria ili kushiriki katika Mkutano wa Saba wa Wakuu wa Nchi Zinazouza Gesi Kwa Wingi Duniani (GECF). Aidha amesema: "Ni safari ya kwanza baada ya miaka 16 kufanyika katika kiwango cha rais wa nchi. Kwa mtazamo wa taifa letu, Algeria ni nchi iliyosimama dhidi ya wakoloni na watu wetu wana kumbukumbu nzuri sana za mapambano ya taifa la Algeria.

Raisi ameitaja nafasi ya Algeria barani Afrika kuwa ni ya kipekee na kuongeza kuwa nchi hii iko katika nafasi muhimu ya ustaarabu wa Kiislamu na uhusiano wa Iran na Algeria unasaidia sana katika uhusiano wetu na Afrika. Aidha amesema nafasi ya Iran na Algeria katika Jumuiya ya Nchi Zinazouza Gesi Kwa Wingi Duniani na katika ulimwengu wa Kiislamu ni nukta mbazo zimezileta nchi hizi mbili karibu zaidi.

Rais wa Iran amsema nukta nyingine ya pamoja baina ya nchi mbili ni mapambano dhidi ya sera za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja katika uga wa kimataifa.

Rais wa Iran akiashiria misimamo ya pamoja ya nchi mbili katika kuwaunga mkono wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina na hasa Gaza amesema: "Bila shaka katika kikao cha pande mbili tutajadili suala la Palestina ambalo hivi sasa si tu kuwa ni suala la ulimwengu wa Kiislamu bali pia ni suala la ubinadamu.

Raisi ameutaja uhusiano wa kisiasa, kibiashara na kiuchumi kuwa ni suala jingine litakalozingatiwa katika safari hii na kusema: "Algeria ni soko zuri sana kwa wafanyabiashara wetu na Iran ya Kiislamu." Aidha amesema kutokana na uhusiano mzuri wa Iran na nchi za Ghuba ya Uajemi na Asia ya Kati, Iran inaweza kutumia nafasi hiyo ya kijiografia kuwanufaisha wafanyabiashara wa Algeria."

Akizungumzia ئkutano wa 7 wa  Saba wa Wakuu wa Nchi Zinazouza Gesi kwa Wingi Duniani, Raisi amesema: “Kikao hiki cha viongozi ni fursa nzuri ya kufuatilia suala kuu la gesi kulingana na mijadala na mapendekezo tuliyoyatoa Doha."

Raisi pia amesema pembezoni mwa mkutano huo atakuwa na vikao na viongozi wengine watakaoshiriki. GECF ina nchi 14 wanachama na viognozi 11 wanatazamiwa kushiriki kikao cha leo jijini Algiers.

4203008

Habari zinazohusiana
captcha