IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini kuwa mwenyeji wa Maonyesho ya Qur'ani Tukufu ya Tehran

11:13 - March 05, 2023
Habari ID: 3476661
TEHRAN (IQNA) – Ukumbi wa Sala (Musalla) wa Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu Amrehemu) utakuwa mwenyeji wa toleo la 30 la Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran, kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Akizungumza katika kipindi cha Idhaa ya Qur'ani ya Iran Jumamosi, Mohammad Mehdi Aziz-Zadeh, ambaye anaongoza sekretarieti ya kudumu ya maonyesho ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, eneo kubwa la Musalla litawekwa kwa ajili ya maonesho hayo mwaka huu na kubainisha kuwa kutakuwa na ongezeko la 30% katika eneo ikilinganishwa na maonesho ya mwaka jana.

Alisema maonyesho hayo yatazinduliwa Aprili 1 (ambayo huenda ikawa siku ya 9 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani) na kuendelea hadi Aprili 15.

Pia alisema baada ya wito kutolewa kwa mawazo mapya na mapendekezo ya kuandaa vyema hafla hiyo ya kimataifa, mawazo tofauti yalipokelewa na kamati ya maandalizi, mawili kati yake yaliamuliwa kutekelezwa katika maonyesho ya mwaka huu.

Mawazo hayo mawili yanahusiana na sehemu ya watoto na vijana ya maonyesho, Aziz-Zadeh alibainisha.

Aidha alibainisha kuwa maonyesho ya mwaka huu yatajumuisha tamasha la chakula ambalo linajumuisha vyakula vya asili, peremende, na vinywaji kutoka sehemu mbalimbali za nchi ambazo ni maalum kwa mwezi mtukufu.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kukuza fikra za Qur'ani Tukufu na kuendeleza shughuli za Qur'ani nchini.

Halikadhalika maonyesho hayo yataweza kuonyesha mafanikio ya hivi punde zaidi ya Qur'ani nchini Iran na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

Baada ya janga hilo kupungua, hafla ya Kurani ilifanyika kibinafsi tena mnamo Aprili 2022 na kauli mbiu ya "Qur'ani Tukufu, Kitabu cha Matumaini na Utulivu".

4125933

Habari zinazohusiana
captcha