Ayatollah Seyyed Ali Khamenei alipokea kundi hilo siku chache zilizopita na habari kuhusu mkutano huo zilisambaza siku ya Alhamisi.
Usomaji wa Qur’ani Tukufu ndani ya kuta za Msikiti wa Mtume (SAW)-Al Masjid An Nabawi, huko Madina ni moja ya "hali nzuri zaidi za kiroho " katika Uislamu, alisema na kuongeza kuwa, "Kuunganishwa Msikiti (Al Masjid An Nabawi) na Qur’anl, na Ka'aba na Qur’ani ni miongoni mwa muunganisho bora zaidi."
"Hilo ni eneo ambalo Qur'ani Tukufu iliteremshwa kwa mara ya kwanza. Ni pale ambapo aya zilianza kuingia katika moyo mtakatifu wa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW). Alisoma aya hizi kwa ulimi wake uliobarikiwa, akizirudia wakati akitufu katika Al-Kaaba. Licha ya kustahimili mateso,kupigwa, na kuteswa, alisoma aya hizi na akaweza kuunda upya historia," Ayatullah Khamenei alisema.
"Kitendo cha kusoma Qur'ani ni njia. Kwa nini? Inatumika kama njia ya kuingiza hekima ya Qur'ani ndani ya moyo, na kwaza kabisa hukuza ukuaji wa jamii ya Kiislamu," aliongeza.
Baada ya kusoma Qur’ani, tuseme, dakika 10 au 15, itakuwa "jambo lenye mvuto" kutumia dakika tano au kumi zinazofuata kutafakari mada za aya zilizosomwa na kuzungumza na hadhirina maana ya aya hizi, alisema Kiongozi Muadhamu.
Hili haliongezei uelewa wao tu bali pia huinua kiwango cha elimu ya hadhirina, amesisitiza.
Kila mwaka mamilioni ya Waislamu kutoka duniani kote hukusanyika Makka kwa ajili ya Hija ambayo kila Mwislamu mwenye uwezo wa kimwili na kifedha anawajibika kuitekeleza angalau mara moja katika maisha yao.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hutuma makumu ya maelefu ya wananchi wake kwenda kushiriki katika ibada ya Hija na kawaida Mahujaji Wairani huandamana na kundi la wanaharakati wa Qur'ani, wanaojulikana kama Msafara wa Nur wa Hija. Mwaka huu msafara huo utaondoka nchini Mei 12 kuelekea Saudi Arabia Mei 15 na kusalai huko kwa takriban siku 40.
Wajumbe wa ujumbe huo wana programu za Qur'ani, ikiwa ni pamoja na vikao vya kusoma Qur'ani kwa vitakavyo jumuisha Mahujaji wa maeneo yote ya dunia katika miji mitakatifu ya Makka na Madina.
4214702