IQNA

Mahujaji Washauriwa Kufuata Miongozo Mipya kuhusu Upigaji Picha

13:50 - June 21, 2023
Habari ID: 3477176
Mahujaji wanaotaka kupiga picha au video kwenye Misikiti Miwili Mitukufu, Msikiti Mkuu wa Makka na Msikiti wa Mtume Muhamad (s.a.w.w) huko mjini Madina, wakati wa Hija lazima wafuate seti mpya ya miongozo iliyotolewa na Wizara ya Hija na Umrah ya Saudi.

 

Wizara ilisema miongozo hii inalenga kuboresha uzoefu wa Hija  na kuhifadhi utukufu  wa maeneo matukufu. Wizara pia imewakumbusha mahujaji kuzingatia sana ibada zao wakati wa ibada ya Hijja. Katika ujumbe wa Twitter, wizara iliwataka mahujaji kuzingatia baadhi ya adabu wanapopiga picha, ili wasisumbue au kuwaumiza mahujaji wengine. Moja ya miongozo kuu ni kuepuka kukaa kwa muda mrefu katika maeneo yenye watu wengi, kwani hii inaweza kuzuia njia ya mahujaji na kuathiri harakati ndani ya maeneo matukufu. Mahujaji pia wanapaswa kujiepusha na njia maalumu na wasizuie mtiririko mzuri wa watu. Zaidi ya hayo, miongozo hiyo inakazia hitaji la kuheshimu faragha ya wengine. Mahujaji wanapewa  moyo wawe waangalifu wanapopiga picha na wasichukue picha zinazoweza kuharibu nafasi za kibinafsi za wanaofanya Ibada zao. Mapendekezo hayo yanakuja huku zaidi ya mahujaji milioni moja wakiwa tayari wamewasili nchini Saudi Arabia kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu huku Saudi Arabia ikiondoa vikwazo ambavyo ilikuwa imeweka kwa idadi ya mahujaji katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kutokana na janga la corona  covid-19.Hija ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya kidini duniani na inachukuliwa kuwa ni wajibu wa kidini ambao ni lazima ukamilike wakati wa uhai wa kila Mwislamu mwenye afya njema na uwezo wa kiuchumi.

 


3484018

 

Kishikizo: hija picha
captcha